Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Gari la kutembelea

 Gari nzuri 
Machapisho ya hivi karibuni

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuuza simu used mtandaoni

 1. Toa maelezo kwa kina pia kuwa mwaminifu Kuna aina mbili za wanunuzi: wale wanaojua wanachotafuta na wale wanaovinjari ili kuona ni nini kinachoweza kuwashawishi. Bila kujali ni aina gani ya mteja unayemuuzia, ni muhimu kila wakati kuwa na maelezo ya kina iwezekanavyo. Usidanganye kuhusu hali au uwezo wa bidhaa yako - kuwa mkweli! Miamala hii ya mtu kwa mtu inategemea uaminifu. Iwapo nitawahi kugundua muuzaji anadanganya kuhusu jambo fulani, kama linavyoweza kuonekana kuwa lisilo na maana, kuna uwezekano kwamba yuko tayari kusema uwongo kuhusu mambo muhimu zaidi, na sitaendelea kushughulika naye. Je, simu mahiri imechakaa, au umeiweka kwenye kipochi tangu siku ya kwanza? Hakikisha kuwaambia watu hali yako na wajulishe ikiwa kuna masuala yoyote. Tafuta mikwaruzo yoyote na uwaambie kile umepata. Amini usiamini, nimeona hii inakupa nafasi nzuri ya kuuza simu, hata ikiwa ina uharibifu zaidi. Wakati watu tayari wana matarajio ya kweli mara ya kwanza wanapoona kifaa ana kwa ana, hawatakat

Biashara ya vyombo vya mtumba

 Ni biashara nzuri sana na inalipa sana muhimu ni wewe uanze, mtaji wake kuanzia 500000 unaanza. Anza kidogo kidogo kwa kusoma mchezo kwanza na uwekeze hatua kwa hatua,usikurupuke tafuta location nzuri pia uza bidhaa original vitu vya plastic wacheki cello ingawa bei juu  tembelea kwenye hayo maduka, omba ukutane na mwenye duka kisha muulize kuhusu biashara hiyo, akiwa na roho nzuri atakupa mchanganuo wote  

Ijue biashara ya vitenge na mtaji wakuanzia nao

 Bashara moja nzuri inawateja wengi sna hasa sehemu za vijiji. challenge hii biaashara. 1)kubali kukopesha 2)Ufatiliaji. 3)minimum polite.language.sbabu mwanamke unamjua akacheka akamalza.mtaji wako.strong language inahitajka mkuu. Business prediodization and time of business. 1)rural and urban. Rural time business. Wakati.wa mavuno kuazia mwezi wa 5hadi wa 8.utapga sna hela mkuu.andaaa.mtaji . urban time business. wakati wote utafanya b iashara. challenges at both businesses zone. 1. Rural . Uaminifu 》lazma.upatemtu mwanifu sna kama utafanya b iashara hiI vijijini. Changamoto ya biashara ya vitenge Changamoto kubwa ni kwenye uuzaji watu wanapokopa kurudisha inakua vigumu hivyo biashara inasuasua. Ila kama ni kwenye minada nadhani siyo ngumu sana kikubwa uwezo wa kupata MZIGO kwa muda muafaka na kuzunguka minadani

Njia za kupata pesa kupitia mtandao

  Hakuna mafanikio yanayokuja kiurahisi, utahitaji juhudi, muda, uvumilivu na kujifunza Zaidi mpaka kupata matokea hivyo usitegemee kupata matokeo ya haraka unapoanza kufanya ishu yoyote mtandaoni. Haya tuangalie njia hizi..... 1. Uhandishi wa maudhui mtandaoni (Online Content writing). Uandishi wa Makala katika Blog na Tovuti (Websites). Kuandaa post kwaajili ya kuweka katika mitandao ya kijamii. Ujuzi unaohitaji • Ujuzi wa kuandika. • Kutambua na kutumia maneno muhimu (keywords). • Uwezo wa kuchambua taarifa. • Kufahamu seo (Search Engine Optimization). 2. Kuuza ujuzi wako mtandaoni kupitia mitandao ya kijamii na freelancing platforms kama Upwork na Fiverr. Juzi unazoweza kuuza mtandaoni • Kutafsiri lugha mbalimbali. • Uandishi wa Makala • Kusimamia mitandao ya kijamii ya watu au kampuni. • Graphic design • Wataalamu wa masuala ya seo • Web design na App developers 3. Udalali /Uuzaji wa ushirika (Affliate marketing). Unapata gawio kwa kuuza bidhaa za watu wengine. Unaweza tumia mitan

Jinsi ya kupata mtaji wa biashara

  Jinsi Ya Kupata mtaji wa biashara tanzania ni Moja kati ya changamoto kabla ya kuanza kufanya biashara au kuanzisha biashara yoyote Katika kipengele hiki naenda kujadili changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye biashara. Jinsi Ya Kupata Mtaji wa Biashara 1. Tumia akiba zako kama mtaji, au anza kuweka akiba. Kama kuna akiba zozote ambazo umekuwa unajiwekea kwa muda unaweza kuzitumia kama mtaji wa kuanzia biashara Kama huna akiba yoyote anza sasa kujiwekea akiba na jipe muda unaohitaji ili kufikisha kiwango cha mtaji unachotaka. 2. Chukua kazi hata yenye maslahi kidogo. Kama ndio umemaliza shule na hujapata ajira na pia huna mshahara wa kuanzia nakushauri uchukue kazi yoyote unayoweza kupata hata kama ina maslahi kidogo. Lengo lako litakuwa ni kukusanya mtaji na hivyo utaifanya kazi hiyo kwa kipindi fulani na kisha kuachana nayo. Inabidi ukubali kuteseka kwa muda kidogo ili uweze kufika kule unakotazamia. Sasa kama utaniambia kwamba wewe ni msomi na kuna kazi

Biashara zinazolipa zaidi Tanzania kwa mtaji mdogo

 Tuangalie biashara 21 za mtaji mdogo usiozidi Tshs. 100,000 unazoweza kufanya na zenye faida kubwa. Mtaji mkubwa unaohitajika unapoanzisha biashara ni muda na wala sio pesa kama utakavyojifunza hapa. 1. KUPIKA KWA  Kama wewe ni mpishi mzuri au una mtu anayejua kupika, basi jitangaze kama unapokea oda za mapishi fulani Tuchukulie unaweza kupika makande au wali nyama vizuri Unachoweza kufanya ni kwenda maofisi ya karibu yako na kuwaambia kwamba wakutafute wanapohitaji hicho chakula wakati wa mchana na wewe utawaletea Usisahau kuacha mawasiliano yako ili waweze kukutafuta Wengi wao watapenda hiyo huduma kwasababu hawatohitaji kutoka tena kufata chakula 2. UREMBO (MAKEUP, KUSUKA & KUCHA Urembo ni gharama. Wanadada wanataka kupendeza wanapokwenda safari zao kama ni kazini ama shughulini Uzuri ni kwamba hii ni biashara ya kila siku unayoweza kufanya Baada ya kufanya utafiti wangu, nimebaini kwamba kufanya makeup, kutengeneza kucha na ususi wa nywele zinalipa vizuri tu Kuna watu wengi tu