Tuangalie biashara 21 za mtaji mdogo usiozidi Tshs. 100,000 unazoweza kufanya na zenye faida kubwa. Mtaji mkubwa unaohitajika unapoanzisha biashara ni muda na wala sio pesa kama utakavyojifunza hapa.
1. KUPIKA KWA
Kama wewe ni mpishi mzuri au una mtu anayejua kupika, basi jitangaze kama unapokea oda za mapishi fulani
Tuchukulie unaweza kupika makande au wali nyama vizuri
Unachoweza kufanya ni kwenda maofisi ya karibu yako na kuwaambia kwamba wakutafute wanapohitaji hicho chakula wakati wa mchana na wewe utawaletea
Usisahau kuacha mawasiliano yako ili waweze kukutafuta
Wengi wao watapenda hiyo huduma kwasababu hawatohitaji kutoka tena kufata chakula
2. UREMBO (MAKEUP, KUSUKA & KUCHA
Urembo ni gharama. Wanadada wanataka kupendeza wanapokwenda safari zao kama ni kazini ama shughulini
Uzuri ni kwamba hii ni biashara ya kila siku unayoweza kufanya
Baada ya kufanya utafiti wangu, nimebaini kwamba kufanya makeup, kutengeneza kucha na ususi wa nywele zinalipa vizuri tu
Kuna watu wengi tu wanaendesha maisha yao kupitia biashara hizo. Kwanini wewe ushindwe? Na kama sio mtaalamu, hakuna tatizo
Chukua muda wako na kujifunza, ndani ya muda utaweza
3. KUUZA JUISI NA ICECREA
Kujifunza kutengeneza juisi au icecream haitakuchukuwa muda mrefu. Ili kufanikiwa katika biashara hii, cha muhimu ni kujitofautisha
Muhimu zaidi unapofanya biashara ya kutengeneza juisi au icecream, ni kuweka mazingira yako safi na salama kwa wateja wako
Uzuri wa biashara hii ni kuwa mtaji wake ni mdogo sana
Elfu kumi tu inatosha kuanzia na wapo waliofanya hivyo na wamekuza biashara zao kama vile Mak Juice au Zanana Juice Box
4. KILIMO CHA MBOGAMBOG
Kilimo ni sehemu kubwa ya maisha ya watanzania na wale wa nchi nyingi za Afrika
Kila siku zikienda, kilimo huzidi kuwa ni biashara ya matajiri kwasababu shamba lina gharama kubwa
Licha ya hivyo, bado kuna fursa ya kutengeneza kipato kupitia kilimo cha mbogamboga hata kama una mtaji mdogo
Anza na sehemu ndogo tu unayoweza kupata hata kama ni nyumbani
5. UFUGAJI WA NDEGE (KUKU, BATA, N.K
Hii ni biashara ambayo ina faida kubwa lakini pia ina changamoto zake kama vile kuku wako kufa
Vifo vya mifugo huwaumiza sana wafugaji na mara nyingi husababishwa na mifugo hiyo kula uchafu
Hivyo, unapoingia kwenye ufugaji jitahidi uwe na mazingira safi na salama kwa mifugo yako
Usafi wa mara kwa mara hasa hasa kwenye malisho yao utahitajika
Kwa vile mtaji ni mdogo, unaweza kuanza na kuku wa kienyeji, bata au hata njiwa. Japo kuwa wanachukuwa muda ila kuwa mvumilivu, faida utaiona
6. KUPIGA PICH
Tangu kuja kwa mitandao ya jamii kama vile Instagram, watumiaji wa mitandao hiyo hutaka picha nzuri
Hapo ndipo unapojitokeza wewe na kuwapa huduma yako ya kupiga picha
Upigaji wa picha ni fani kama fani yengine, ili ujitofautishe pendelea kujifunza kwa wanaojua au tumia YouTube kujifunza
Vifaa vya upigaji picha vina gharama ila sio lazima viwe vyako, muhimu ni kuwa na ujuzi. Vifaa unaweza kumuazima rafiki yako au kukodi
7. KUTENGENEZA TOVUTI (WEBSITES
Tuko katika ulimwengu wa habari na teknolojia, hivyo kampuni ama biashara ambayo hawako mtandaoni wanakosa wateja
Ichangamkie fursa hiyo kwa kujifunza kutengeneza websites kupitia YouTube
Kisha, tafuta biashara/ makampuni ambayo hawana tovuti na uwaelezee umuhimu wa kuwa na tovuti
Mwisho, waambie kuwa wewe unatoa huduma hiyo
Kwa kuanza, wateja wako wa mwanzo unaweza kuwafanyia kwa bei ya punguzo halafu mbeleni ukapandisha. Njia hii itakusaidia kupata mabalozi watakao kupatia wateja wengine
8. KUPANGA SHEREHE/MATUKIO (EVENT PLANNING
Kuanzia maharusi, kitchen party, sandoff na sherehe nyenginezo nisizozifahamu. Zote hizi ni fursa ambapo unaenda kusaidia watu kuandaa sherehe zao mwanzo mpaka mwisho
Wewe ndio unaumiza kichwa kutafuta watu na huduma mbalimbali kama vile wapambaji, ma dj, au kuwatafutia gari ya kukodi, kuwapikishia chakula na megine mengi
Unachohitaji kuweza kufanya biashara hii ni uwe unawajua watu husika wanaotakiwa kwenye sherehe hizo
Mfano, ujue wapambaji wa ukumbi, wapishi wa maharusi, ma dj ili uweze kuwapa kazi hizo. Utalipwa kwa kufanya kazi hiyo
9. KUTEMBEZA WATALI
Hii nayo ni biashara nyengine ambayo haihitaji pesa kabisa
Unachohitaji ni kufahamu historia ya nchi yako hasa hasa ile ya maeneo ambayo watalii wanapenda kwenda
Mfano, Zanzibar mtembeza watalii anaweza kulipwa kuanzia elfu ishirini kwa safari moja. Kwa siku ukipata safari tano tu unaondoka na zaidi ya laki moja
10. USHONAJI NGU
Kama wewe ni mpenzi wa mitindo, unaweza tengeneza kipato kizuri kwa kuwashonea watu nguo
Itakuchukuwa muda kujifunza kushona ila ni kazi moja nzuri. Unapata kuwa mbunifu katika kutengeneza mishono mbali mbali na mwisho wake kulipwa
Kama huna cherehani nyumbani, unaweza kwenda kukodi na kufanyia kazi zako hadi utakapo nunua yako
11. KUFUNDISH
Unaweza kufundisha chochote kila unachokijua ikiwa kuna watu wanataka kujifunza
Jitathmini kwa kujiuliza, je ni kitu gani nakijua ambacho watu wanataka kujifunza? Hiyo ni rasilimali tosha
Watafute hao watu na uwape huduma zako. Taaluma sio lazima iwe kufundisha hesabati na kemia tu, kama unajua kupika vizuri, kushona au chochote kile basi wafundishe watu
12. KUTENGENEZA SIMU/KOMPYUT
Watumiaji wa vifaa kama vile simu na kompyuta huzidi kila siku
Vifaa hivi vinapopata tatizo kama vile kuingia loki sio kila mtu anaweza kutengeneza mwenyewe
Hiyo hukupa wewe fursa ya kuwatatulia matatizo yao kwa kiasi cha pesa kadhaa. Unaweza kujifunza jinsi ya kutengeneza matatizo sugu ya simu kwenye mtandao
13. UNYOZI WA NYWEL
Hii pia ni biashara isiyokuwa na msimu kwavile nywele huota kila siku
Jifunze kunyoa watu nywele halafu anza na wale wakaribu yako kama vile marafiki na ndugu
Utakapofanya kazi nzuri hao watakuwa wateja wako wakujirudia na pia kukutangazia huduma zako kwa watu wengine
Unachohitaji ni kununua mashine ya kunyolea ambayo unaweza kupata kwa chini ya elfu hamsini
14. KUNUNUA NA KUUZA BIDHA
Sifa ya kubwa ya mjasiriamali ni kuona thamani ya vitu kabla wengine hawajaviona
Hivyo, tafuta bidhaa ambazo zinauzwa kwa bei ya chini, zinunue na utafute soko ambalo hizo bidhaa zinauzwa kwa bei ya juu uende ukaziuze huko
Mfano, unaweza kutoa bidhaa Dar es Salaam ukaja kuuza Zanzibar na kinyume chake pia inawezekana
15. KUUZA VOCHA ZA SIM
Vocha! Tunanunua karibia kila siku
Faida yake sio kubwa kihivyo ila ukizingatia kazi ni ndogo ya kufanya kwasababu vocha zinajiuza wenyewe
Vocha sio kitu cha kutumia nguvu kuuza muhimu watu wajue tu kama unauza vocha
Unaweza kuona vocha zinauzwa kila sehemu kwamba utakosa wateja … lakini sio kweli, kuna sehemu nyingi tu ambazo hakuna muuza vocha karibu
Anza kuwauzia watu unaoishi nao, majirani au hata wanafunzi wa chuo
16. UFUGAJI WA SAMAK
Ufugaji wa samaki uko wa aina mbili, kuna samaki wa kula na wale wa mapambo. Hapa nitaongelea samaki wa mapambo kwa vile wana gharama ndogo na pia faida kubwa
Unaweza anza na samaki wawili au wanne na kuwatunza. Wakizaliana na kuwa wengi, uza baadhi yao
17. KUKUZA MITI YA MAU
Maua hupendezesha nyumba na wengi huamua kupanda nyumbani kwao
Fuatilia jinsi gani maua tofauti yanavyopandwa na kisha yapande
Kwa wastani, mti mmoja wa maua huuzwa kuanzia elfu mbili. Mtaji mkubwa hapa ni muda wa kupanda na kuishughulikia hiyo miti
18. KUFANYA USAFI MAJUMBANI NA MAOFISIN
Watu wengi wamebanwa na kazi, na muda wasiokuwa kazini wana mambo mengi ya kufanya
Unaweza kuwafanyia usafi na wakakulipa. Ni vizuri ukanunua vifaa vyako ambavyo sio ghali ila sehemu nyingi watakuruhusu kutumia vifaa vyao vya usafi
Biashara ikiwa kubwa, unaweza amua kutafuta vifaa tofauti tofauti vya kufanyia kazi kitaalamu zaidi
19. KOCHA WA MAZOEZ
Nathubutu kusema kuwa hakuna kitu chenye thamani kwenye maisha kama afya nzuri
Watu wengi wanashtuka sikuhizi juu ya umuhimu wa kula vizuri na kufanya mazoezi. Hivyo, baada ya kupata elimu nzuri ya mazoezi, anza kawafundisha watu. Utalipwa kwa ujuzi na muda wako
20. KUPAMBA MAHARUS
Harusi ni biashara kubwa
Hivi, nani hapendi kupendeza siku ya harusi yake? Hamna. Na ili kupendeza harusini, wanandoa inabidi wapambwe
Tafuta mtu anayepamba maharusi na muombe kumfanyia kazi (ikiwezekana bila hata malipo). Baada ya muda utajifunza vitu vingi vitakavyo kusaidia kuwa mtaalamu wa kupamba maharusi
21. KUWAUZIA WATU BIDHAA ZA
Kwa akili ya kawaida, ni rahisi mtu kukulipa unapomtengenezea pesa
Jifuze kuuza kisha tafuta watu wenye biashara na uwaambie kuwa unaweza kuwaletea wateja kwa malipo mutakayokubaliana
Hii ni biashara nzuri kwasababu unatengeneza kipato kwa kutumia fedha ya mtu mwengine. Unachohitaji ni ujuzi wa kuuza vitu..O...I..I...I...A..I.....U...A....E...A...A...O...I....).....)....A.....)....A....M.....).....ODAasababu unatengeneza kipato kwa kutumia fedha ya mtu mwengine. Unachohitaji ni ujuzi wa kuuza vitu.
Maoni
Chapisha Maoni