Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Njia mbalimbali za kuandika tangazo la biashara

Ikiwa ni mfanyabiashara jifunze jinsi ya kuwashawishi wateja na kupata matokeo.unatakiwa kutangaza kupata matokeo makubwa watu wavutiwe na bidhaa zako na kuwafanya wateja kuwa na hamu kubwa ya kununua bidhaa zako

Jifunze njia mbalimbali za kuandika tangazo la kuuza bidhaa/huduma mtandaoni
1.Andika kama vile jinsi unavyoongea
Kampuni yako au bidhaa yako ni kama mtu na inasifa yakuwa na sauti. Na tumia hiyo sauti kuifuatisha
Andika tangazo kama vile unavyoweza kuzungumza,maneno utayoandika kati ya kampuni yako na mnunuzi wako
Sauti yako na hasa maneno utayochagua kutumia yatakuwa tofauti sana

2.Andika sifa na faida kabla haujaanza
Watu hawawezi kununua bidhaa yako au huduma yako ikiwa hawafahamu watanufaika na nini kwenye bidhaa yako. Mfano unauza  printer waelimishe watu huduma yako itawasaidiaje, je inaokoa mda na kazi?
Ubora wa hiyo bidhaa yako?
Unamwambia nini mteja ategemee kwenye hiyo bidhaa?
Andika sifa na faida kwa mteja kile ambacho atanufaika kuhusu bidhaa au huduma yako

3.Andika kile unachokiona. Fanya mawasiliano moja kwa moja na waambie kwanini wateja ni muhimu sana kwako na kitu gani utafanya kwa ajili ya wateja wako. Vitu vya kutilia mkazo nikuwaeleza
Kipi wataweza kukipata
Utatafuta cha kuwapa
Watawez kuona

4.Tumia sentensi za vitendo
Matokeo na vitendo huwa havitokei vyenyewe. Watu wanafanya na matokeo yanatokea
Mfano kama unauza alarm unawez ukaandika tangazo lako hivi
"Linda familia yako na mali zako kuzuia uvunjaji kwa kutumia alarm zetu za ulinzi
Ina uwezo mkubwa anza leo kuzitumia kuliko kuendelea  "kupoteza mali,kupoteza maisha  na kupata majeraha ondoa tatizo hilo kwa kutumia alarm zetu za ulinzi
"
5.Nenda mbele zaidi ili kuwaunganisha
Wafanye wasomaji washiriki miongozo yako kutoka wazo moja kwenda lingine. Tumia maneno kama haya

Nini cha zaidi..

Lakuongezea...

Pia muhimu..

Vizuri hata hivyo...

Kumbuka...

Unaweza pia..

La mwisho...

Jumlisha...


6.Onesha ni jinsi gani bidhaa/huduma itatua tatizo la mteja
Linapokuja swala la kuandika kichwa cha habari,Wafanyabiashara wengi wanakosea kuandika kichwa cha habari. Hichi ndio kitu cha kwanza mtu anakisoma
Kichwa cha habari ndio sehemu muhimu kwako kufanikisha ili mteja asome tangazo lako
Watu huwa wanafungua tangazo ambalo wanaona litatatua matatizo yao
Kabla hauja andika tangazo angalia ni jinsi gani kichwa cha habari kitawasaidia watu kutatua matatizo yao

7.Toa ofa
Hii ni sehemu itayokusaidia kukufungulia biashara kuanza kufanya mauzo. Pia ni sehemu ambayo tangazo lako litazidi kuwa kubwa kwanini? Sababu matangazo mengi yanayotangazwa na wafanyabiashara hayatoi ofa mfano kama unauza nguo katika tangazo lako utaweza kuandika
"Ndani ya msimu huu wa sikukuu tunatoa ofa kwenu wateja wetu kutakuwa na punguzo kubwa la bei zaidi ya asilimia 20"
Vitu vya kuzingatia unavyotoa ofa
Toa ofa bidhaa ambayo watu wanahitaji sana
Toa ofa ambayo thamani ya bidhaa/huduma viendane

8. Watoe hofu wateja
Ikiwa umemaliza kazi yako ya kuandika tangazo lako kuna kitu kingine pia unaweza ukakifanya . Watu hawawezi kununua kwa sababu tatu

-Wanaogopa kupoteza pesa
-Hawana usibitisho kwa hicho unachowaambia kama ni sahihi
-Hawahitaji huduma yako

Njia nzuri ya kuweza kuondoa hofu kwa wateja nikuwapa huduma yako bure kwa mda mfupi kama ofa ili wapate uhakika na kile unachowaambia pia

Anza leo kuanza kutangaza bidhaa zako hapa guliotanzania.com



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi ya kuuza nyumba yako haraka mtandaoni

Linapokuja swala la kuuza nyumba kitu cha kuzingatia ni kupata dalali mzuri wa nyumba na majengo ambaye unaona anauelewa wa kutosha Na leo hii Gulio Tanzania tupo hapa tumekuorodhoshea hatua saba mambo ya kuyazingatia unapotaka kuuza nyumba mtandaoni 1.Fanya utafiti sifa za dalali unayemfikiria kukuuzia nyumba yako Kabla haujachagua dalali unayempenda hakikisha unampata dalali ambaye atakuuzia nyumba kwa bei nzuri pia awe mwaminifu 2.Chukua mda kuandaa picha Kitu cha msingi wanunuaji wa nyumba mtandaoni wanachokiangalia zaidi ni picha kabla hawajataka kujua vitu vingine kazi kwako kuchukua picha za nyumba yako zenye muonekano mzuri Chukua picha ya nyumba nzima kwa mbele ambayo itaonekana bila gari au wanyama pia chukua picha ikionesha vyumba,sebule kama kuna yard ya magari au swimming pool 3.Usisahau kulipia kiasi kidogo tangazo lako premium listing Hatua ya kwanza kabisa kuuza nyumba yako mtandaoni ni rahisi kama tangazo lako litakuwa ukurasa wa mbele ambao wanunuaji ...

Jifunze mbinu za kuuza bidhaa za jumla kwa wauzaji wa rejareja

Jifunze mbinu za kuuza bidhaa za jumla kwa wauzaji wa rejareja Leo hii tumeandaa makala kwa ajili yenu wauzaji wa jumla,wasambazaji wakubwa Lakini wawe wanauza jumla hatujawasau leo tutawapa muongozo jinsi ya kuuza jumla kwa wauzaji wa rejareja Jinsi ya kuuza bidhaa za jumla kwa wateja wa rejareja 1.UTAANZIA KUUZA BEI GANI UNAYOIFIKIRIA Hii ni sehemu muhimu sana kwa muuzaji wa jumla ambayo hautakiwi kufanya mchezo ni vizuri unapo uza bidhaa yako hakikisha bei ya kawaida kabisa ya kuuzia mzigo unauza bei 2.5x ya gharama za mzigo Hii bei ya jumla ikuletee nusu ya faida ya mzigo wote Mfano kama gharama za bidhaa ni elfu 20000 kwa muuzaji wa rejareja utamuuzia kwa bei ya 60000 hapo pigia pamoja nagharama ya usafiri,masoko na gharama zingine Inabidi pia uwe na kianzio cha kuuza bidhaa zako na kama muuzaji atachukua bidhaa nyingi na bei itapungua mfano kama unauza screen protector kama unaanzia kuuza kwanzia piece 100 bei itakuwa Tsh 3000 ila kama mnunuzi atataka kwanzia piece 5...