Hakuna mafanikio yanayokuja kiurahisi, utahitaji juhudi, muda, uvumilivu na kujifunza Zaidi mpaka kupata matokea hivyo usitegemee kupata matokeo ya haraka unapoanza kufanya ishu yoyote mtandaoni.
Haya tuangalie njia hizi.....
1. Uhandishi wa maudhui mtandaoni (Online Content writing).
Uandishi wa Makala katika Blog na Tovuti (Websites).
Kuandaa post kwaajili ya kuweka katika mitandao ya kijamii.
Ujuzi unaohitaji
• Ujuzi wa kuandika.
• Kutambua na kutumia maneno muhimu (keywords).
• Uwezo wa kuchambua taarifa.
• Kufahamu seo (Search Engine Optimization).
2. Kuuza ujuzi wako mtandaoni kupitia mitandao ya kijamii na freelancing platforms kama Upwork na Fiverr.
Juzi unazoweza kuuza mtandaoni
• Kutafsiri lugha mbalimbali.
• Uandishi wa Makala
• Kusimamia mitandao ya kijamii ya watu au kampuni.
• Graphic design
• Wataalamu wa masuala ya seo
• Web design na App developers
3. Udalali /Uuzaji wa ushirika (Affliate marketing).
Unapata gawio kwa kuuza bidhaa za watu wengine.
Unaweza tumia mitandao yako ya kijamii au kuwa na blog ama Tovuti (Website) maalumu kwaajili ya kuuzia bidhaa hizo.
4. Uza bidhaa zako binafsi mtandaoni.
Jifunze kuuza mtandaoni kisha anza kuuza bidhaa au huduma yako mtandaoni.
Inaweza kuwa huduma pia kuuza mtandaoni inawezekana na wateja wengi kwasasa wapo mitandaoni hivyo ni rahisi kuwafikia ikiwa utakuwa na mbinu sahihi za kuwatafuta.
Maoni
Chapisha Maoni