Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Jinsi ya kupata mtaji wa biashara

 Jinsi Ya Kupata mtaji wa biashara tanzania ni Moja kati ya changamoto kabla ya kuanza kufanya biashara au kuanzisha biashara yoyote Katika kipengele hiki naenda kujadili changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye biashara.

Jinsi Ya Kupata Mtaji wa Biashara

1. Tumia akiba zako kama mtaji, au anza kuweka akiba.


Kama kuna akiba zozote ambazo umekuwa unajiwekea kwa muda unaweza kuzitumia kama mtaji wa kuanzia biashara Kama huna akiba yoyote anza sasa kujiwekea akiba na jipe muda unaohitaji ili kufikisha kiwango cha mtaji unachotaka.


2. Chukua kazi hata yenye maslahi kidogo.


Kama ndio umemaliza shule na hujapata ajira na pia huna mshahara wa kuanzia nakushauri uchukue kazi yoyote unayoweza kupata hata kama ina maslahi kidogo. Lengo lako litakuwa ni kukusanya mtaji na hivyo utaifanya kazi hiyo kwa kipindi fulani na kisha kuachana nayo. Inabidi ukubali kuteseka kwa muda kidogo ili uweze kufika kule unakotazamia. Sasa kama utaniambia kwamba wewe ni msomi na kuna kazi huwezi kufanya, nitakuambia uendelee kuimba tatizo ni mtaji.


3. Anza kidogo.


Unapoanza biashara hasa pale unapoanzia sifuri ni vigumu sana kuweza kupata kiasi chote cha fedha unachohitaji. Unaweza kuanza kidogo na baadae ukaendelea kukua na pia kujifunza. Jua ni kiasi gani unahitaji kama mtaji na gawa kwenye kiasi kidogo ambacho unaweza kuanzia. Ukisema usubiri mpaka upate kiasi kikubwa unachofikiria itakuchukua muda mrefu sana na baadae utakata tamaa.


4. Ungana na mwenzako mwenye mawazo kama yako.


Unaweza kuungana na mwenzako au wenzako wenye mawazo kama yako na mkaunganisha fedha kidogo mlizo nazo na kuzifanya kama mtaji ili kuweza kuanza biashara. Hii ni njia nzuri sana ya kuweza kuunganisha mitaji kidogo ambayo unaweza kuitumia na ukafikia mafanikio makubwa.

5. Uza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa navyo ili kupata mtaji.


Kama unataka kuanza biashara ila huna mtaji, nakushauri uuze vitu vingi ambavyo ulinunua ukiwa masomoni ambavyo kwa sasa hauna uhitaji mkubwa navyo ili kupata mtaji, biashara yako itakurudishia na zaidi. Ukipiga mahesabu ya haraka haraka unaweza kupata kiasi fulani cha fedha kinachotosha kuanzia kama utauza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa kwa sasa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Njia mbalimbali za kuandika tangazo la biashara

Ikiwa ni mfanyabiashara jifunze jinsi ya kuwashawishi wateja na kupata matokeo.unatakiwa kutangaza kupata matokeo makubwa watu wavutiwe na bidhaa zako na kuwafanya wateja kuwa na hamu kubwa ya kununua bidhaa zako Jifunze njia mbalimbali za kuandika tangazo la kuuza bidhaa/huduma mtandaoni 1.Andika kama vile jinsi unavyoongea Kampuni yako au bidhaa yako ni kama mtu na inasifa yakuwa na sauti. Na tumia hiyo sauti kuifuatisha Andika tangazo kama vile unavyoweza kuzungumza,maneno utayoandika kati ya kampuni yako na mnunuzi wako Sauti yako na hasa maneno utayochagua kutumia yatakuwa tofauti sana 2.Andika sifa na faida kabla haujaanza Watu hawawezi kununua bidhaa yako au huduma yako ikiwa hawafahamu watanufaika na nini kwenye bidhaa yako. Mfano unauza  printer waelimishe watu huduma yako itawasaidiaje, je inaokoa mda na kazi? Ubora wa hiyo bidhaa yako? Unamwambia nini mteja ategemee kwenye hiyo bidhaa? Andika sifa na faida kwa mteja kile ambacho atanufaika kuhusu bidhaa au hu...

Jinsi ya kuuza nyumba yako haraka mtandaoni

Linapokuja swala la kuuza nyumba kitu cha kuzingatia ni kupata dalali mzuri wa nyumba na majengo ambaye unaona anauelewa wa kutosha Na leo hii Gulio Tanzania tupo hapa tumekuorodhoshea hatua saba mambo ya kuyazingatia unapotaka kuuza nyumba mtandaoni 1.Fanya utafiti sifa za dalali unayemfikiria kukuuzia nyumba yako Kabla haujachagua dalali unayempenda hakikisha unampata dalali ambaye atakuuzia nyumba kwa bei nzuri pia awe mwaminifu 2.Chukua mda kuandaa picha Kitu cha msingi wanunuaji wa nyumba mtandaoni wanachokiangalia zaidi ni picha kabla hawajataka kujua vitu vingine kazi kwako kuchukua picha za nyumba yako zenye muonekano mzuri Chukua picha ya nyumba nzima kwa mbele ambayo itaonekana bila gari au wanyama pia chukua picha ikionesha vyumba,sebule kama kuna yard ya magari au swimming pool 3.Usisahau kulipia kiasi kidogo tangazo lako premium listing Hatua ya kwanza kabisa kuuza nyumba yako mtandaoni ni rahisi kama tangazo lako litakuwa ukurasa wa mbele ambao wanunuaji ...

Jifunze mbinu za kuuza bidhaa za jumla kwa wauzaji wa rejareja

Jifunze mbinu za kuuza bidhaa za jumla kwa wauzaji wa rejareja Leo hii tumeandaa makala kwa ajili yenu wauzaji wa jumla,wasambazaji wakubwa Lakini wawe wanauza jumla hatujawasau leo tutawapa muongozo jinsi ya kuuza jumla kwa wauzaji wa rejareja Jinsi ya kuuza bidhaa za jumla kwa wateja wa rejareja 1.UTAANZIA KUUZA BEI GANI UNAYOIFIKIRIA Hii ni sehemu muhimu sana kwa muuzaji wa jumla ambayo hautakiwi kufanya mchezo ni vizuri unapo uza bidhaa yako hakikisha bei ya kawaida kabisa ya kuuzia mzigo unauza bei 2.5x ya gharama za mzigo Hii bei ya jumla ikuletee nusu ya faida ya mzigo wote Mfano kama gharama za bidhaa ni elfu 20000 kwa muuzaji wa rejareja utamuuzia kwa bei ya 60000 hapo pigia pamoja nagharama ya usafiri,masoko na gharama zingine Inabidi pia uwe na kianzio cha kuuza bidhaa zako na kama muuzaji atachukua bidhaa nyingi na bei itapungua mfano kama unauza screen protector kama unaanzia kuuza kwanzia piece 100 bei itakuwa Tsh 3000 ila kama mnunuzi atataka kwanzia piece 5...