Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mambo ya kuzingatia unavyotaka kuuza smartphone mtandaoni


Wengi wetu huwa tunapenda kuziuza smartphone zetu hasa pale tunaposikia kuna toleo jipya limeingia
Lakini sio kitu kirahisi. Ni wazo zuri kufikiria kuuza simu uliyoitumia kwa mda mrefu ili uweze kupunguza  gharama za kununua simu toleo jipya kila siku

Kuuza na kununua simu nyingine itakusaidia kupunguza gharama
Uuzaji wa simu ni kama sayansi. Kuna watu wengi wanaishi kwa kutegemea biashara hii.Kuna wengine wamesomea biashara hii kwa miaka

Nimeuza na kununua simu mtandaoni kwa kupata mafanikio makubwa ndo mana leo nimeleta makala hii kwa wale ambao hawana uzoefu waweze  kujua mambo ya kuzingatia ili waweze kujifunza
Mambo ya kuzingatia unavyotaka kuuza smartphone mtandaoni

1.Toa maelezo ya simu kwa kina na kuwa mwaminifu
Kuna aina mbili za wateja kuna wa wale ambao wanatafuta bidhaa ili wanunue lakini kuna wale ambao baada ya kuperuzi mtandaoni wakavutiwa na bidhaa
Bila kujali ni kundi lipi unaloliuzia bidhaa hakikisha kila mara unakuwa na maelezo ya bidhaa zako.Usidanganye kuhusu hali ya simu yako au uwezo
Biashara inahitaji uaminifu ikiwa utamuuzia mteja bidhaa na akagundua kuna kitu muuzaji umemdanganya ata kama kidogo hapo tayari hatorudi tena kwako kutaka bidhaa zako
Endapo kava la smartphone yako limechakaa au kava haujalibadilisha tangia mara ya kwanza unanunua simu 
Hakikisha unamwambia mteja hali ya simu yako unamfanya ajue kama kuna tatizo lolote.Angalia kama kuna scratches yoyote kwenye simu mwambie 
Amini usiamini ukifanya hivi itakupa nafasi nzuri za kuuza simu ata kama inamatatizo mengi akiwa tayari na matarajio ya ukweli kwa mara ya kwanza alivyoiona bidhaa yako awezi kukataa
Ila kama ataona sratches,mikwaluzo na matatizo mengine lakini wewe haukumwambia hapa ujue kuna uwezekano mkubwa mteja kutoendelea kufanya biashara na wewe

Pia penda kuwaambia watu simu yako inafanyaje kazi. Inaweza ikachukua sehemu ya kazi yako,wanunuzi wengi ni wakawaida na hawana habari zote kuhusu mambo ya kiufundi.Wao hawafikiri simu yako inafanyaje kazi.chakufanya wewe wape kile maelezo kidogo unachokijui kuhusu simu yako ambacho kitakuwa na msaada
Kitu gani kitafanya gani uuze simu yako?

Kama muuzaji orodhesha specification za simu yako vile unavyofikiri pendelea pia kureview ili kujua specification za simu yako

Na mnunuzi atataka kujua kwanini unaiuza smartphone yako .Unataka upate simu nyingine kama hiyo yenye uwezo mkubwa?Unatafuta simu nyingine mpya? Hauipendi
?
2.Muda ni pesa
Kumbuka smartphone zinamuda mfupi sana siku hizi
Smartphone nyingi zinaonekana kama ni za zamani kwa miezi michache tu kwahiyo wahi kuziuza smartphone kabla hazijapitwa na wakati. Usinunue simu leo ukaaitumia muda mrefu na ukategemea utamuuzia mtu baadae! Jinsi unavyokaa nayo mda smartphone na ndo jinsi thamani yake inavyoshuka
Jaribu kuuza simu kabla halijatolewa toleo lingine la smartphone hiyo
Watu huwa wanapenda kusikia simu wanazonunua ni toleo jipya kutoka kiwandani
Kama ni muuzaji unaposikia tetezi kwamba hiyo kampuni ya simu yako inataka kutoa tokeo jingine la simu hiyo huo ndio muda mzuri wa kuiuza simu hiyo uliyonayo kwa bei nzuri ili upate smartphone toleo jipya

3.Wapi unaweza ukaiuza smartphone yako
Sasa unajua unaweza kuuza kupitia internet,huu ni muda unaweza kwenda mbele zaidi na weka simu yako online
Tunapendekeza utumie tovuti ya guliostore.com au  app ya Gulio Store kuuza simu zako na bidhaa nyingine nyingi 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Njia mbalimbali za kuandika tangazo la biashara

Ikiwa ni mfanyabiashara jifunze jinsi ya kuwashawishi wateja na kupata matokeo.unatakiwa kutangaza kupata matokeo makubwa watu wavutiwe na bidhaa zako na kuwafanya wateja kuwa na hamu kubwa ya kununua bidhaa zako Jifunze njia mbalimbali za kuandika tangazo la kuuza bidhaa/huduma mtandaoni 1.Andika kama vile jinsi unavyoongea Kampuni yako au bidhaa yako ni kama mtu na inasifa yakuwa na sauti. Na tumia hiyo sauti kuifuatisha Andika tangazo kama vile unavyoweza kuzungumza,maneno utayoandika kati ya kampuni yako na mnunuzi wako Sauti yako na hasa maneno utayochagua kutumia yatakuwa tofauti sana 2.Andika sifa na faida kabla haujaanza Watu hawawezi kununua bidhaa yako au huduma yako ikiwa hawafahamu watanufaika na nini kwenye bidhaa yako. Mfano unauza  printer waelimishe watu huduma yako itawasaidiaje, je inaokoa mda na kazi? Ubora wa hiyo bidhaa yako? Unamwambia nini mteja ategemee kwenye hiyo bidhaa? Andika sifa na faida kwa mteja kile ambacho atanufaika kuhusu bidhaa au hu...

Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi ya mafuta kwa wateja wa jumla

Makampuni mengi lengo lao kubwa ni kuuza bidhaa zao za mafuta ya ngozi jumla kwa wateja wanaoenda kuuza rejareja. Hatua hii inaweza kuwa changamoto kwa wazalishaji wa bidhaa na wauzaji ili uweze kufanya mauzo vizuri na ufanikiwe kuwapata wanunuzi wa bidhaa yako inatakiwa ufanye maandalizi na ujue nini unategemea Kufanikiwa kufikisha na kuuza bidhaa za mafuta ya ngozi kwa wanunuaji fuata hatua chache na kuwa na ujuzi .kiujumla kampuni inaweza kuwa kubwa ,ikawepo mtandaoni lakini watu wangapi nao wanafanya hivyo Weka mipango vizuri kuhusu wateja,ushindani,na brand izidi kukuwa. Pia kuwa makini wakati wa kuuza na kufanya mapatano ya bei. Mwisho biashara yako itakuwa na itapanuka Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi kwa bei ya jumla 1. Wanunuaji huwa wanaangalia bidhaa yenye ubunifu Inatakiwa uuze bidhaa ambayo mtu atataka kununua . Pengine inaweza ikawa na ubunifu katika kifungashio,vitu vilivyotumika kutengenezea,technolojia,inavyotumika etc  inatakiwa uongeze t...

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni

Kuna watu wengi wanauza magari kupitia mtandao wanatangaza biashara kupitia mitandao mikubwa hapa Tanzania kama guliostore.com , Kupatana na ZoomTanzania, na   ni njia ya kupata wateja wengi zaidi baada ya kuchagua tovuti ya kutaka kutangaza biashara  osha gari lako kisha chukua picha nyingi zakupost mtandaoni Kama mteja atakutafuta utamwambia maongezi ya bei utofauti wa bei na wauzaji wenzio itategemea na gari yako ina hali gani Hapa leo tumekuletea mambo yakuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni 1.Hakikisha una kadi ya gari Mara unavyoweka gari lako mtandaoni wateja wengi wataanza kukutafuta. Kabla haujaanza kutangaza mtandaoni hakikisha gari yako unavielelezo vyote kuwa wewe ndio mmiliki pia lipia mapato yako yote ikiwa kama unadaiwa 2.Elewa kipi unakijua kuhusu gari yako Mara mtu anapoanza kukutafuta huwa anakuja na maswali mengi utafanya  vizuri kuwajibu Ikiwa hauna ujuzi wowote ni muda sasa wakuanza kufuatilia gari yako ina engine ya aina g...