Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Jifunze mbinu za kuuza bidhaa za jumla kwa wauzaji wa rejareja


Jifunze mbinu za kuuza bidhaa za jumla kwa wauzaji wa rejareja
Leo hii tumeandaa makala kwa ajili yenu wauzaji wa jumla,wasambazaji wakubwa
Lakini wawe wanauza jumla hatujawasau leo tutawapa muongozo jinsi ya kuuza jumla kwa wauzaji wa rejareja

Jinsi ya kuuza bidhaa za jumla kwa wateja wa rejareja

1.UTAANZIA KUUZA BEI GANI UNAYOIFIKIRIA
Hii ni sehemu muhimu sana kwa muuzaji wa jumla ambayo hautakiwi kufanya mchezo ni vizuri unapo uza bidhaa yako hakikisha bei ya kawaida kabisa ya kuuzia mzigo unauza bei 2.5x ya gharama za mzigo
Hii bei ya jumla ikuletee nusu ya faida ya mzigo wote
Mfano kama gharama za bidhaa ni elfu 20000 kwa muuzaji wa rejareja utamuuzia kwa bei ya 60000 hapo pigia pamoja nagharama ya usafiri,masoko na gharama zingine
Inabidi pia uwe na kianzio cha kuuza bidhaa zako na kama muuzaji atachukua bidhaa nyingi na bei itapungua mfano kama unauza screen protector kama unaanzia kuuza kwanzia piece 100 bei itakuwa Tsh 3000 ila kama mnunuzi atataka kwanzia piece 500 utauza bei ya Tsh 2000 kwa kila piece moja

2.Tafuta wateja unaowalenga unaotaka bidhaa zako ziwafikie

Fanya utafiti wateja wapi unaowalenga? bidhaa yako utauzia wapi? na je kuna ushindani wa bidhaa zako? na mikoa ipi unayofikilia kuiuzia bidhaa zako, majibu ya maswali yako yote utayapata bidhaa zako unazionaje kwenye soko la ushindani wa wauzaji wengine
Zaidi chagua muuzaji wa rejareja wakufanya nae kazi

 3.JIFUNZE KUJIONDOA KWENYE USHINDANI WA SOKO
Fikiria pale unapochagua mgawaha wa kula chakula pengine kilichokuvutia zaidi ni sifa za mgahawa kuliko hata chakula ni cha wastani tu
Hata kwenye bidhaa zako unaweza ukafanya hivi kuwa tayari kumfanya mnunuzi awe shuhuda kuwa bidhaa yako ni bora.unapoanza kuuza mtandaoni unakuwa haujulikani wala hauna sifa zozote anza kutoa ofa bure kama sample kwa bidhaa zako kwa wateja, waulize kutaka kujua maoni
Pale utapopata feedback nzuri utakuwa unajiweka tofauti kwenye soko la ushindani
Watu wanapokuwa wamekuamini unaweza ukaanza kuandika makala zinazoendana na bidhaa zako kutoa muongozo kwa wauzaji wa rejareja

4.Usisahau kujenga brand
Kumbuka wewe ni muuzaji wa jumla na wateja wako wauzaji rejareja usiwekeze pesa nyingi kwenye kufanya mauzo utakuwa unakosea kumbuka wateja huwa wananunua bidhaa ambazo wanahisi wanaweza wakauza vile ambavyo bidhaa inavyokuwa inauzika zaidi sokoni ndivyo ambavyo wateja watazidi kununua kwako
Kumbuka kujenga brand kuna mambo mengi yatakayokusaidia kujenga brand ya kampuni yako

5.Jiandae kwa mapokeo
Mapokeo ni sehemu ya kujifunza kuuza jumla
Bidhaa zako haiwezi kuwa fit kwa kila muuzaji wa rejareja atavutiwa. Jiandae kwanza kabla hausambaza mzigo mkubwa kwa wateja
Mapokeo yanaweza yakajitokeza nje ya bidhaa yako
Pengine mzigo ulikuwa nao ukawa mkubwa sana kuliko idadi ya wateja au soko likawa halipo msimu huo
Usikate tamaa kuhusu mapokeo ni wakati wakuweza kujifunza

6.Badilika kuendana na soko linavyohitaji
Ikiwa umefanya mauzo makubwa usiishie hapo angalia mbele zaidi na angalia kipi unahitaji kukibadilisha. Ingia mtandaoni angalia washindani wako pitia sifa na bidhaa za washindani wako ambazo ni sawa na zako na angalia ni namna gani unaweza ukaboresha huduma yako na bidhaa
Wapi unataka kuelekea kwa bidhaa yako inayokuja sokoni nenda na wakati ili kufanya biashara yako izidi kukuwa

7.Tumia tovuti maarufu kutangaza bidhaa zako
mfano kama tovuti ya
Gulio Store
Inawafikia maelfu ya wauzaji na wanunuzi mtandaoni
Inajulikana na watu wengi
Kutangaza bidhaa yoyote ni bure
Malipo wanayotoza kwa premium ni kiasi kidogo tangazo lako litaoneka ukurasa wa mbele wa tovuti hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kuuza bidhaa zako
Anza sasa kutangaza bidhaa ingia guliostore.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Njia mbalimbali za kuandika tangazo la biashara

Ikiwa ni mfanyabiashara jifunze jinsi ya kuwashawishi wateja na kupata matokeo.unatakiwa kutangaza kupata matokeo makubwa watu wavutiwe na bidhaa zako na kuwafanya wateja kuwa na hamu kubwa ya kununua bidhaa zako Jifunze njia mbalimbali za kuandika tangazo la kuuza bidhaa/huduma mtandaoni 1.Andika kama vile jinsi unavyoongea Kampuni yako au bidhaa yako ni kama mtu na inasifa yakuwa na sauti. Na tumia hiyo sauti kuifuatisha Andika tangazo kama vile unavyoweza kuzungumza,maneno utayoandika kati ya kampuni yako na mnunuzi wako Sauti yako na hasa maneno utayochagua kutumia yatakuwa tofauti sana 2.Andika sifa na faida kabla haujaanza Watu hawawezi kununua bidhaa yako au huduma yako ikiwa hawafahamu watanufaika na nini kwenye bidhaa yako. Mfano unauza  printer waelimishe watu huduma yako itawasaidiaje, je inaokoa mda na kazi? Ubora wa hiyo bidhaa yako? Unamwambia nini mteja ategemee kwenye hiyo bidhaa? Andika sifa na faida kwa mteja kile ambacho atanufaika kuhusu bidhaa au hu...

Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi ya mafuta kwa wateja wa jumla

Makampuni mengi lengo lao kubwa ni kuuza bidhaa zao za mafuta ya ngozi jumla kwa wateja wanaoenda kuuza rejareja. Hatua hii inaweza kuwa changamoto kwa wazalishaji wa bidhaa na wauzaji ili uweze kufanya mauzo vizuri na ufanikiwe kuwapata wanunuzi wa bidhaa yako inatakiwa ufanye maandalizi na ujue nini unategemea Kufanikiwa kufikisha na kuuza bidhaa za mafuta ya ngozi kwa wanunuaji fuata hatua chache na kuwa na ujuzi .kiujumla kampuni inaweza kuwa kubwa ,ikawepo mtandaoni lakini watu wangapi nao wanafanya hivyo Weka mipango vizuri kuhusu wateja,ushindani,na brand izidi kukuwa. Pia kuwa makini wakati wa kuuza na kufanya mapatano ya bei. Mwisho biashara yako itakuwa na itapanuka Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi kwa bei ya jumla 1. Wanunuaji huwa wanaangalia bidhaa yenye ubunifu Inatakiwa uuze bidhaa ambayo mtu atataka kununua . Pengine inaweza ikawa na ubunifu katika kifungashio,vitu vilivyotumika kutengenezea,technolojia,inavyotumika etc  inatakiwa uongeze t...

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni

Kuna watu wengi wanauza magari kupitia mtandao wanatangaza biashara kupitia mitandao mikubwa hapa Tanzania kama guliostore.com , Kupatana na ZoomTanzania, na   ni njia ya kupata wateja wengi zaidi baada ya kuchagua tovuti ya kutaka kutangaza biashara  osha gari lako kisha chukua picha nyingi zakupost mtandaoni Kama mteja atakutafuta utamwambia maongezi ya bei utofauti wa bei na wauzaji wenzio itategemea na gari yako ina hali gani Hapa leo tumekuletea mambo yakuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni 1.Hakikisha una kadi ya gari Mara unavyoweka gari lako mtandaoni wateja wengi wataanza kukutafuta. Kabla haujaanza kutangaza mtandaoni hakikisha gari yako unavielelezo vyote kuwa wewe ndio mmiliki pia lipia mapato yako yote ikiwa kama unadaiwa 2.Elewa kipi unakijua kuhusu gari yako Mara mtu anapoanza kukutafuta huwa anakuja na maswali mengi utafanya  vizuri kuwajibu Ikiwa hauna ujuzi wowote ni muda sasa wakuanza kufuatilia gari yako ina engine ya aina g...