Kuuza nguo kwa jumla imekuwa ni biashara yenye faida ni fursa inayokuwa kila mwaka. Kila mtu huwa anatafuta brand za nguo maarufu zinazouzwa kwa bei ndogo. Wauzaji wengi wana njia wanazozitumia siku zote kuuza bidhaa
Japokuwa soko la mtandaoni limekuwa ni njia rahisi sana kuuza nguo za jumla na soko linafanya vizuri .
Uza nguo za jumla
Unaweza ukauza nguo za jumla kwa tovuti ya guliostore.com
Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza nguo za jumla mtandaoni
1.Chagua aina ya nguo
Huwezi kumuhudumia kila mtu chagua aina ya nguo iwe moja au mbili tu unazotaka kuuza mtandaoni kama utambulisho wako kwa wanunuzi kama unauza magauni hakikisha ni magauni tu usichanganye na nguo nyingine lakini utofauti uwepo kwenye size ukawa na gauni za kuvaliwa malika yote
2.Nguo zinapotoka
Hapa Waambie watu nguo zako zinatoka wapi,ubora wa hizo nguo na brand ya hiyo nguo
3.Chukua picha zinazovutia upande wa nyuma na mbele ya nguo pia na label
Mara unapokuwa una nguo anza kuchukua picha. Napendekeza kuchukua kamera nzuri kufanyia kazi chukua picha ya mbele na nyuma ya nguo
Pia piga picha ya maelezo yoyote ambayo yameprintiwa kwenye nguo
Hakikisha unachukua picha ya label yeyote ya nguo na picha ya maelezo. kuonesha size ya nguo
4.Downlod vipimo vya brand ya nguo weka pamoja na picha
Ni rahisi kutafuta vipimo vya nguo mtandaoni uta google jina la brand na vipimo vyake
Utapakia pamoja na picha hii itakusaidia pale wateja watapotaka kukuuliza kutaka kujua ukweli kuhusu vipimo vya nguo unayouza
5.Tumia model kuwaonyesha watu mavazi yako
Watu huwa wanapenda kuona nguo imevaliwa
hivi karibuni nilinunua jaketi mtandaoni lakini nikaja kuona kola ni kubwa sana
Kwahiyo ukitaka kuuza nguo mtandaoni tumia mbinu yakuweka picha ikimuonesha model wako kavaa pia utaweka na maelezo kwamba nguo yako inaweza kuvaliwa mahali gani hii ni njia ambayo mnunuzi atashawika kununua
6.pendelea kupost bidhaa zako mwisho wa wiki
Kama unatumia tovuti za kuuza na kununua bidhaa kama guliostore.com fatilia kwa siku ambazo watu wengi wanakuwa online siku za weekend hasa jumapili watu wengi wapo online hii itakufanya uuze nguo kwa bei nzuri na watu wakakutafuta tofauti na ukipost bidhaa zako siku ya jumatatu au jumanne
7.Andika maelezo yatakayomshawishi mnunuaji
Fikiria kila mnunuzi ata nunua kutoka na maelezo yako tu uliyoandika hapo kabla hajaona picha. Maelezo yawe kiufupi
Ikiwa hauna uhakika na nguo unayouza ipoje ni rahisi fatilia kupitia kutafuta google kuna picha nyingi zinataja mitindo
8.Chukua vipimo vya nguo
Pima nguo zako kwaajili ya kuuza mtandaoni wateja wanapenda kujua vipimo vya urefu,upana,na unene unaweza ukaongeza vipimo vya nguo kwenye maelezo yako ya bidhaa yako
9.unganisha bei ya bidhaa na gharama za usafiri
Unavyouza nguo zako utaweka bei ya juu ili kufidia gharama za usafiri lakini mteja atakapo kuwa anataka kununua bidhaa utamwambia usafiri ni bure
10.Jenga mahusiano mazuri na wateja
Wateja watakapo kufuata watakuuliza maswali mengi kuwa na furaha kuyajibu hata kama hanunui mda huo pengine atanunua awamu nyingine
Endapo utakuwa umeshayajibu maswali yako,weka maswali hayo mbele ya ukurasa wako wa social network ili na wateja wengine wayaone
11.Mfanye mteja ajue tayari umeshatuma mzigo na umeshapokea pesa yake
Mara unapokuwa umeshafanya mauzo hakikisha mteja anajua tayari umeshapata pesa
Unavyokuwa unatuma mjulishe kuwa umetuma
12.Mfanye mteja akumbuke huduma yako
Kila mauzo unayofanya hakikisha unakuwa na business card unaweza kuipata kwa bei rahisi na pia unakuwa na logo ili iwe rahisi mteja kukutafuta
13.Andaa nguo zingine kuwauzia tena wateja
Mara unapokuwa umeuza bidhaa kumbuka kuwarudia wateja wa nyuma pengine wanaweza wakapenda nguo zako nyingine kwahiyo ni vizuri kuwa na bidhaa nyingine za kuwaonesha na kuwa natumaini watanunua tena
14.Tumia tovuti maarufu kutangaza bidhaa zako
mfano kama tovuti ya
Gulio Store
Inawafikia maelfu ya wauzaji na wanunuzi mtandaoni
Inajulikana na watu wengi
Kutangaza bidhaa yoyote ni bure
Malipo wanayotoza kwa premium ni kiasi kidogo tangazo lako litaoneka ukurasa wa mbele wa tovuti hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kuuza bidhaa zako
Anza sasa kutangaza bidhaa ingia guliostore.com


Maoni
Chapisha Maoni