Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Jinsi ya kufanikiwa katika biashara

 Kuanzisha biashara Tanzania huambatana na changamoto kadhaa kama ukosefu wa mtaji na mkakati dhaifu wa uuzaji. Lakini badala ya kuangalia sababu zinazofanya biashara kushindwa, napenda tujikite katika makala hii kwenye mambo yanayoweza kufanikisha biashara inayoanzishwa. Mawazo haya nimeyagawanya katika dondoo zifuatazo.

Tazama biashara za maeneo jirani unayoishi au biashara za watu unaowafahamu. Je, ni mambo gani yaliyofanya biashara hizo kufanikiwa, kubaki vilevile kwa muda mrefu, au hata kushindwa? Ni sababu zipi zimeleteleza matokeo hayo?

Kwa hakika kuna sababu nyingi,  zikiwemo sababu binafsi ambazo ziko nje ya uewelewa wetu. Kwa msingi huo hatuwezi tukadai kujua sababu za kila biashara kushindwa. Hata hivyo, napenda tutazame baadhi ya mambo muhimu yanayopelekea biashara kufanikiwa au hata kushindwa.

  1. Mkakati dhabiti wa uuzaji. Watanzania wanafahamu kutumia fursa katika kufanya biashara zao. Hii huusisha kufungua biashara katika maeneo yalio na watu wengi, au karibu ya kaya zao ambapo wanaweza kuduhumia kaya za jirani kwa bidhaa na huduma huku wakitimiza majukumu yao ya nyumbani. Popote pale biashara yako ilipo, ili ikue na ifanikiwe, inapaswa kujikita katika kutimiza hitaji flani la watu walioko katika eneo hilo.  Hivyo shauku ya kuanzisha biashara na kujishughulisha haina budi kuambatana na mahitaji ya msingi ya watu katika eneo husika. Ili kuweza kujua mahitaji ya wateja wako wa baadaye na kufanya uamuzi mzuri wa aina ya biashara ya kuendesha, unapaswa kufanya utafiti wa soko.
  2. Naamini unafahamu tabia ya baadhi ya watu kuelekea katika fursa flani ya biashara na kubadili mwelekeo, yaani biashara, pale wanapoona fursa nyingine. Ni kweli kuwa kupata uzoefu katika biashara tofauti tofauti huleta manufaa. Hata hivyo, swala la kubadili badili biashara lapaswa kutathminiwa kwa kina, hasa pale ambapo matokeo yake yanaathiri kipato cha familia. Kwa hakika jambo hili tunalitazama kwa utofauti, iwapo mtu ana kipato thabiti kutokana na ajira, chenye kukidhi mahitaji yake na familia yake huku “akijijaribu” katika biashara flani. Kutimiza wajibu wa riziki yako na familia yako ni muhimu huku ukijikita katika biashara yako kwa uvumilivu na kutafuta mafanikio katika biashara hiyo.
  3. Udhibiti mzuri wa mtaji. Nimekutana na baadhi ya wanafanyabiashara wanaotumia pesa au bidhaa za biashara kwa ajili ya matumizi yao binafsi (k.v. kwa ajili chakula, nauli au dharura). Hili jambo, hata kama wakati flani halikwepeki, linahitaji nidhamu kubwa. Ikarimu unaweza kuhatarisha biashara yako. Kutenganisha matumizi ya biashara na matumizi binafsi ni jambo la msingi sana. Ni kweli kuwa upatikanaji wa mtaji ni muhimu katika kuanzisha biashara. Mtu achukuaye mkopo kwa ajili ya mtaji anapaswa kutuambua deni analodaiwa na umuhimu wa kulipa deni hilo, ukizingatia kuwa kipindi cha awali cha biashara huwa kinaambatana na hasara. Kiasi kikubwa cha mkopo humaanisha pia kiasi kikubwa cha deni na kiasi kikubwa cha deni huweza kupelekea kushindwa kulipa kama pesa haidhibitiwi vizuri au ikijitokeza hasara kubwa kutoka na mauzo au wizi. Kama unakusudia kuanzisha biashara ndogo, fikiria kuhusu biashara zisizohitaji mtaji au zinazohitaji mtaji mmdogo. Kumbuka methali inayosema: “Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe” . Jipatie mawazo kupitia mtandao au marafiki kuhusu aina za biashara zisizohitaji mkopo au zinazohitaji mkopo mdogo. Unaweza kuwasiliana nasi kwa mawazo zaidi.
  4. Jifunze kuboresha biashara yako. Kimsingi, ni vema kupata maarifa ya biashara hata kabla ya kuanza biashara. Unaweza kuona wepesi wa kufanya biashara, lakini kuwa mnyenyekevu ili kujifunza zaidi na kuepuka makosa ya kibiashara, kunaweza kukusogeza mbele zaidi. Kama umeshaanza biashara yako, jipatie muda, utoke katika mihangaiko ya biashara yako, ili ujifunze namna ya kuiboresha. Kutana na wanafanyabiashara wengine wazoefu zaidi na waliofanikiwa, pata ushauri kutoka benki, jiunge katika jukwaa la majidala au tafuta mshauri wa kitaalam ili ujifunze kutokana na uzoefu wa wengine na changamoto zao. Unaweza kufaidika sana.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Njia mbalimbali za kuandika tangazo la biashara

Ikiwa ni mfanyabiashara jifunze jinsi ya kuwashawishi wateja na kupata matokeo.unatakiwa kutangaza kupata matokeo makubwa watu wavutiwe na bidhaa zako na kuwafanya wateja kuwa na hamu kubwa ya kununua bidhaa zako Jifunze njia mbalimbali za kuandika tangazo la kuuza bidhaa/huduma mtandaoni 1.Andika kama vile jinsi unavyoongea Kampuni yako au bidhaa yako ni kama mtu na inasifa yakuwa na sauti. Na tumia hiyo sauti kuifuatisha Andika tangazo kama vile unavyoweza kuzungumza,maneno utayoandika kati ya kampuni yako na mnunuzi wako Sauti yako na hasa maneno utayochagua kutumia yatakuwa tofauti sana 2.Andika sifa na faida kabla haujaanza Watu hawawezi kununua bidhaa yako au huduma yako ikiwa hawafahamu watanufaika na nini kwenye bidhaa yako. Mfano unauza  printer waelimishe watu huduma yako itawasaidiaje, je inaokoa mda na kazi? Ubora wa hiyo bidhaa yako? Unamwambia nini mteja ategemee kwenye hiyo bidhaa? Andika sifa na faida kwa mteja kile ambacho atanufaika kuhusu bidhaa au hu...

Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi ya mafuta kwa wateja wa jumla

Makampuni mengi lengo lao kubwa ni kuuza bidhaa zao za mafuta ya ngozi jumla kwa wateja wanaoenda kuuza rejareja. Hatua hii inaweza kuwa changamoto kwa wazalishaji wa bidhaa na wauzaji ili uweze kufanya mauzo vizuri na ufanikiwe kuwapata wanunuzi wa bidhaa yako inatakiwa ufanye maandalizi na ujue nini unategemea Kufanikiwa kufikisha na kuuza bidhaa za mafuta ya ngozi kwa wanunuaji fuata hatua chache na kuwa na ujuzi .kiujumla kampuni inaweza kuwa kubwa ,ikawepo mtandaoni lakini watu wangapi nao wanafanya hivyo Weka mipango vizuri kuhusu wateja,ushindani,na brand izidi kukuwa. Pia kuwa makini wakati wa kuuza na kufanya mapatano ya bei. Mwisho biashara yako itakuwa na itapanuka Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi kwa bei ya jumla 1. Wanunuaji huwa wanaangalia bidhaa yenye ubunifu Inatakiwa uuze bidhaa ambayo mtu atataka kununua . Pengine inaweza ikawa na ubunifu katika kifungashio,vitu vilivyotumika kutengenezea,technolojia,inavyotumika etc  inatakiwa uongeze t...

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni

Kuna watu wengi wanauza magari kupitia mtandao wanatangaza biashara kupitia mitandao mikubwa hapa Tanzania kama guliostore.com , Kupatana na ZoomTanzania, na   ni njia ya kupata wateja wengi zaidi baada ya kuchagua tovuti ya kutaka kutangaza biashara  osha gari lako kisha chukua picha nyingi zakupost mtandaoni Kama mteja atakutafuta utamwambia maongezi ya bei utofauti wa bei na wauzaji wenzio itategemea na gari yako ina hali gani Hapa leo tumekuletea mambo yakuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni 1.Hakikisha una kadi ya gari Mara unavyoweka gari lako mtandaoni wateja wengi wataanza kukutafuta. Kabla haujaanza kutangaza mtandaoni hakikisha gari yako unavielelezo vyote kuwa wewe ndio mmiliki pia lipia mapato yako yote ikiwa kama unadaiwa 2.Elewa kipi unakijua kuhusu gari yako Mara mtu anapoanza kukutafuta huwa anakuja na maswali mengi utafanya  vizuri kuwajibu Ikiwa hauna ujuzi wowote ni muda sasa wakuanza kufuatilia gari yako ina engine ya aina g...