Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuanzisha biashara

 Tunakutana tena leo katika safu yetu ya kuhabarishana habari njema, na mafundisho yatakayokutoa sehemu moja kwenda sehem nyingine kifikra na kiuchumi, napenda kusema tu kusoma tu peke yake haitoshi ila kusoma na kuweka kwenye matendo ulichokisoma ndio msaada mkubwa wa mafanikio yako.


Leo tutajadili pamoja mambo manne ambayo unatakiwa kuzingatia kabla hujaanza biashara, huenda ulikuwa una wazo la kuanzisha biashara lakini bado hujui yapi ya kufanya mwanzo kabla ya kuanza biashara. Twende wote hadi mwisho wa makala haya utajifunza kitu;

1. WATU: Kitu cha kwanza cha kuzingatia unapowaza kuanzisha biashara ni watu, nadhani unajua kabisa kuwa huwezi kuanzisha biashara bila kuwepo watu, kumbe watu ndio rasilimali pekee unayoweza kuifikiria kabla hujaanza biashara yako, kwa sababu bila watu hakuna mauzo.

Tunapozungumzia watu kwenye biashara tunazungumzia watu wa aina mbili;

(A) Wateja wako.
(B) Watu wanaofanyabiashara kama yako.

WATEJA WAKO - Kitu cha kwanza unapotaka kuanzisha biashara lazima ujue wateja wako ni kina nani? Watoto, watu wazima, wanawake, wanaume au wazee. Unapotambua wateja wako ni watu wa aina gani itakupa urahisi mzuri wa wewe kujua utawapataje, hebu jiulize kama leo unataka kuanzisha biashara ya bidhaa za urembo halafu kazi yako ni kutembelea sehemu walioko wanaume tu eti kisa watawapelekea wake zao itakula kwako, lazima utakapotaka kuanzisha biashara ufahamu ni wateja wako ni watu gani utajuwa kwa kuwapata maisha yako yatakuwa rahisi.

WATU WANAOFANYABISHARA KAMA YAKO - Watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika biashara kwa sababu ya kuanzisha biashara kwa kuiga, kwa sababu umemuona jirani yako kafungua duka anauza na wewe una mihela yako ya mkopo tayari unaanza na wewe kwenda kufungua duka kama lile pembeni yake, matokeo yake hupati wateja, unajua kitakachokukuta, utakuwa mara kwa mara unaenda kujipitisha kwenye duka lake unaangalia labda kuna kitu tofauti ameweka unakuta ni vile vile kama kwako, unajiuliza mbona wewe huuzi?

Rafiki utamaliza soli za viatu bure ulikosea njia, watu wanaofanya biashara kama yako ni kuhimu sana usijenge nao uadui, kama unajijua unapenda kufanya biashara ya kuuza mahindi hebu kabla hujaanza jenga urafiki na mtu anaefanya biashara kama hiyo, akishakuwa rafiki yako anza kumuuliza kidogo kidogo kwa ustaarabu, alianzaje, anapata wapi yeye mahindi na kwa bei ipi, je na wewe ukitaka kuanza anakushauri uanzaje?

Atakupa mbinu ambazo zitakusaidia katika biashara na utakuwa sana na utaona wapi pakuanzia, usifikiri kuwa na mtaji mkubwa ndio kufanikiwa katika biashara, unaweza kuanza na elfu ishirini tu na ukatengeneza mabilioni. Mfano nilipoanza biashara na Neptunus nilikuwa sina mtaji kabisa mkubwa lakini 26000 ilianza kunipa mwanya wa kuwa na mtaji mkubwa hadi kuwashinda walioamini watafanikiwa kwa mitaji yao.

2. BIDHAA: Kitu cha pili cha kuangalia ni bidhaa yako, jiulize swali moja "bidhaa yako ni mpya au tayari kuna watu wengine tayari wameshaianza?" Kama ni mpya unaweza ianza kwa ubora unaoweza wewe kwa sababu hakuna alieanzisha na ukaboresha kutokana na matakwa ya wateja, lakini kama bidhaa yako tayari kuna watu wengine wanayo, rafiki hapa ndipo utajua neno mjasiriamali lina maana gani, unatakiwa kuwa makini sana.

Lazima ukafanye utafiti waliotangulia bidhaa yao ina ubora gani, Ili wewe uweke ubora unaozidi kiwango, hiki ndicho huwa kinanifurahisha kwenye semina nyingi zinazofundisha ujasiriamali eti wanawafundisha watu kutengeneza sabuni itakayoshindana na mbuni au jamaa bila kuwaambia viwango vya sabuni hizo, matokeo yake watanzania wamebaki wanasoma kama fasheni bila mafanikio.

Hakikisha bidhaa yako ni bora kuliko zilizotangulia utauza sana, usikalie kuumiza kichwa kuzalisha bidhaa nyingi, umiza kichwa kuzalisha bidhaa bora.

3. MAHALI PA KUUZIA: Kitu cha tatu unachotakiwa kujua ni sehemu ambayo biashara yako itakaa, umejua watu, umeshaboresha bidhaa yako, unachotakiwa sasa nikujua wapi biashara yako itakaa? Ukikosea pa kuweka biashara yako ndugu yangu utakula hadi mtaji.

Hebu fikiria unafungua bureau de change (biashara ya kuchenji hela) Tandale kwa Mtogole, kweli hata kama biashara yako inahitaji watu hapo utakuwa umechemka, unafungua supermarket BUGURUNI NDANI NDANI kweli utauza? Hapana, nakushauri hakikisha biashara yako umeiweka kwa watu sahihi na mahali sahihi utapata faida kubwa na utakuwa tajiri muda sio mrefu.

4. BEI YA BIDHAA: Kitu cha mwisho unachotakiwa kuangalia ni bei za bidhaa zako, ndugu unaetaka kuanzisha biashara hebu jiulize bei za bidhaa zako na watu husika vinalingana, na tatizo kubwa la wafanyabiashara wengi hawajui jinsi ya kupanga bei kwenye bidhaa zao. Kama mfanyabiashara, lazima ujue jinsi ya kupanga bei za bidhaa zako Mungu akipenda siku zijazo tutafundisha jinsi ya kupanga bei, bei ikiwa kubwa hutauza bidhaa, ikiwa ndogo hutapata faida na biashara itakufa.

Unapotaka kupanga bei lazima uangalie na watu husika, wewe ukauze shati la elfu tano ukaliuze Tandale elfu ishirini eti kisa frame yako umeandika classic, hutauza ng'oo, kuwa mjanja, bei zako ziendane na sehemu husika, muda mwingine ni bora upate faida kidogo lakini biashara izunguke, biashara inapokaa sana dukani tayari inashuka thamani hata ukiiuza tayari thamani yake inakuwa imeshuka.

Hivyo unapotaka kuwa mfanyabiashara angalia bei za bidhaa zako na watu husika. Me huwa nawapenda sana wamachinga, ukienda kitu cha elfu kumi anakuanzia elfu ishirini halafu anakupa uhuru wa kupunguza anajua kabisa utapunguza hadi elfu kumi na tano, ukinunua mwingine akija kitu kile kile cha elfu kumi anauziwa elfu tano, kumbe tayari kuna mtu ameshamlipia elfu tano.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Njia mbalimbali za kuandika tangazo la biashara

Ikiwa ni mfanyabiashara jifunze jinsi ya kuwashawishi wateja na kupata matokeo.unatakiwa kutangaza kupata matokeo makubwa watu wavutiwe na bidhaa zako na kuwafanya wateja kuwa na hamu kubwa ya kununua bidhaa zako Jifunze njia mbalimbali za kuandika tangazo la kuuza bidhaa/huduma mtandaoni 1.Andika kama vile jinsi unavyoongea Kampuni yako au bidhaa yako ni kama mtu na inasifa yakuwa na sauti. Na tumia hiyo sauti kuifuatisha Andika tangazo kama vile unavyoweza kuzungumza,maneno utayoandika kati ya kampuni yako na mnunuzi wako Sauti yako na hasa maneno utayochagua kutumia yatakuwa tofauti sana 2.Andika sifa na faida kabla haujaanza Watu hawawezi kununua bidhaa yako au huduma yako ikiwa hawafahamu watanufaika na nini kwenye bidhaa yako. Mfano unauza  printer waelimishe watu huduma yako itawasaidiaje, je inaokoa mda na kazi? Ubora wa hiyo bidhaa yako? Unamwambia nini mteja ategemee kwenye hiyo bidhaa? Andika sifa na faida kwa mteja kile ambacho atanufaika kuhusu bidhaa au hu...

Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi ya mafuta kwa wateja wa jumla

Makampuni mengi lengo lao kubwa ni kuuza bidhaa zao za mafuta ya ngozi jumla kwa wateja wanaoenda kuuza rejareja. Hatua hii inaweza kuwa changamoto kwa wazalishaji wa bidhaa na wauzaji ili uweze kufanya mauzo vizuri na ufanikiwe kuwapata wanunuzi wa bidhaa yako inatakiwa ufanye maandalizi na ujue nini unategemea Kufanikiwa kufikisha na kuuza bidhaa za mafuta ya ngozi kwa wanunuaji fuata hatua chache na kuwa na ujuzi .kiujumla kampuni inaweza kuwa kubwa ,ikawepo mtandaoni lakini watu wangapi nao wanafanya hivyo Weka mipango vizuri kuhusu wateja,ushindani,na brand izidi kukuwa. Pia kuwa makini wakati wa kuuza na kufanya mapatano ya bei. Mwisho biashara yako itakuwa na itapanuka Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi kwa bei ya jumla 1. Wanunuaji huwa wanaangalia bidhaa yenye ubunifu Inatakiwa uuze bidhaa ambayo mtu atataka kununua . Pengine inaweza ikawa na ubunifu katika kifungashio,vitu vilivyotumika kutengenezea,technolojia,inavyotumika etc  inatakiwa uongeze t...

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni

Kuna watu wengi wanauza magari kupitia mtandao wanatangaza biashara kupitia mitandao mikubwa hapa Tanzania kama guliostore.com , Kupatana na ZoomTanzania, na   ni njia ya kupata wateja wengi zaidi baada ya kuchagua tovuti ya kutaka kutangaza biashara  osha gari lako kisha chukua picha nyingi zakupost mtandaoni Kama mteja atakutafuta utamwambia maongezi ya bei utofauti wa bei na wauzaji wenzio itategemea na gari yako ina hali gani Hapa leo tumekuletea mambo yakuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni 1.Hakikisha una kadi ya gari Mara unavyoweka gari lako mtandaoni wateja wengi wataanza kukutafuta. Kabla haujaanza kutangaza mtandaoni hakikisha gari yako unavielelezo vyote kuwa wewe ndio mmiliki pia lipia mapato yako yote ikiwa kama unadaiwa 2.Elewa kipi unakijua kuhusu gari yako Mara mtu anapoanza kukutafuta huwa anakuja na maswali mengi utafanya  vizuri kuwajibu Ikiwa hauna ujuzi wowote ni muda sasa wakuanza kufuatilia gari yako ina engine ya aina g...