Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mambo yakuzingatia unapotaka kuanzisha biashara ya chakula (mgahawa)

 Mgahawa ni moja kati ya biashara zinazolipa hapa nchini. Kutokana na hilo, hakuna urahisi katika biashara hii kuanzia kwa mmiliki hadi wafanyakazi. Na ili watu wapende kula katika mgahawa wako unatakiwa kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa ikiwa ni pamoja na usafi, muonekano wa mgahawa wako n.k.

Kama umeamua kufanya biashara hii zingatia haya:

  • Si kila mtu lazima awe mmiliki wa mgahawa

Unapenda kupika? Vizuri, unapenda kula? Vizuri zaidi, unapenda kuburudisha? Jambo zuri lakini hayo yote hayawezi kukufanya uwe na vigezo vya kumiliki  mgahawa. Mambo unayotakiwa kuzingatia ni pamoja na je unapenda kufanya kazi masaa mengi? Unaweza kumudu kutolipwa kwa muda? Unaweza kununua bima ya afya? Na sio kufikiria tu kufungua biashara. Wazo la kuwa bosi ni zuri lakini linakuja na majukumu mengi kuliko unavyoweza kufikiria.

ADVERTISEMENT
  • Eneo

Kati ya vitu muhimu kwenye biashara hii ni eneo. Hutakiwi kupuuzia swala hili kwasababu eneo likiwa zuri uhakika wa kupata wateja wengi ni mkubwa na kufungua mgahawa eneo baya kutakwamisha ndoto zako za kuwa na mgahawa kwa muda mrefu. Hivyo kama una wazo la eneo ambalo unaweza kufungua mgahawa wako fanya utafiti na kuwa tayari kuuanzisha mgahawa katika eneo tofauti.

  • Hakuna mgahawa wa bei rahisi

Inategemea na ukubwa, mandhari ya mgahawa wako mpya unatakiwa kujua kuwa biashara ya mgahawa haianzishwi kwa fedha  ndogo. Unatakiwa kujipanga na kuhakikisha una fedha za kutosha kwa ajili ya uanzilishi wa mgahawa wako. Hivyo  unatakiwa kuandika kila kitu kinachohitaji fedha na kuandika pembeni kama unaweza kumudu gharama za mambo yote kwa kiasi gani ili uweze kufanya maamuzi sahihi.

  • Dhana (concept) ya mgahawa ni muhimu

Dhana ya mgahawa itakuongoza katika mambo mengi ya mgahawa wako ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa orodha ya vyakula na bei (menu), muonekano wa mgahawa, na jina la mgahawa. Kila muanzilishi wa mgahawa siku zote hutaka mgahawa wake kuwa wa kipekee na bora zaidi kuliko migahawa mingine. Hivyo usichanganye mambo sababu utawapa wateja wako wakati mgumu na kuwafanya kwenda sehemu nyingine.

  • Mpango wa biashara

Kwa sababu biashara ya mgahawa mzuri inahitaji mtaji mkubwa, hivyo ni muhimu kuwa na mpango wa biashara ikitokea utahitaji wawekezaji wa nje kuja kuwekeza katika mgahawa wako. Aidha, mpango wa biashara ni muhimu kwa mtu ambaye anamiliki biashara kwa mara ya kwanza kwa kuwa itamsaidia kujua muelekeo wa biashara yake.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Njia mbalimbali za kuandika tangazo la biashara

Ikiwa ni mfanyabiashara jifunze jinsi ya kuwashawishi wateja na kupata matokeo.unatakiwa kutangaza kupata matokeo makubwa watu wavutiwe na bidhaa zako na kuwafanya wateja kuwa na hamu kubwa ya kununua bidhaa zako Jifunze njia mbalimbali za kuandika tangazo la kuuza bidhaa/huduma mtandaoni 1.Andika kama vile jinsi unavyoongea Kampuni yako au bidhaa yako ni kama mtu na inasifa yakuwa na sauti. Na tumia hiyo sauti kuifuatisha Andika tangazo kama vile unavyoweza kuzungumza,maneno utayoandika kati ya kampuni yako na mnunuzi wako Sauti yako na hasa maneno utayochagua kutumia yatakuwa tofauti sana 2.Andika sifa na faida kabla haujaanza Watu hawawezi kununua bidhaa yako au huduma yako ikiwa hawafahamu watanufaika na nini kwenye bidhaa yako. Mfano unauza  printer waelimishe watu huduma yako itawasaidiaje, je inaokoa mda na kazi? Ubora wa hiyo bidhaa yako? Unamwambia nini mteja ategemee kwenye hiyo bidhaa? Andika sifa na faida kwa mteja kile ambacho atanufaika kuhusu bidhaa au hu...

Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi ya mafuta kwa wateja wa jumla

Makampuni mengi lengo lao kubwa ni kuuza bidhaa zao za mafuta ya ngozi jumla kwa wateja wanaoenda kuuza rejareja. Hatua hii inaweza kuwa changamoto kwa wazalishaji wa bidhaa na wauzaji ili uweze kufanya mauzo vizuri na ufanikiwe kuwapata wanunuzi wa bidhaa yako inatakiwa ufanye maandalizi na ujue nini unategemea Kufanikiwa kufikisha na kuuza bidhaa za mafuta ya ngozi kwa wanunuaji fuata hatua chache na kuwa na ujuzi .kiujumla kampuni inaweza kuwa kubwa ,ikawepo mtandaoni lakini watu wangapi nao wanafanya hivyo Weka mipango vizuri kuhusu wateja,ushindani,na brand izidi kukuwa. Pia kuwa makini wakati wa kuuza na kufanya mapatano ya bei. Mwisho biashara yako itakuwa na itapanuka Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi kwa bei ya jumla 1. Wanunuaji huwa wanaangalia bidhaa yenye ubunifu Inatakiwa uuze bidhaa ambayo mtu atataka kununua . Pengine inaweza ikawa na ubunifu katika kifungashio,vitu vilivyotumika kutengenezea,technolojia,inavyotumika etc  inatakiwa uongeze t...

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni

Kuna watu wengi wanauza magari kupitia mtandao wanatangaza biashara kupitia mitandao mikubwa hapa Tanzania kama guliostore.com , Kupatana na ZoomTanzania, na   ni njia ya kupata wateja wengi zaidi baada ya kuchagua tovuti ya kutaka kutangaza biashara  osha gari lako kisha chukua picha nyingi zakupost mtandaoni Kama mteja atakutafuta utamwambia maongezi ya bei utofauti wa bei na wauzaji wenzio itategemea na gari yako ina hali gani Hapa leo tumekuletea mambo yakuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni 1.Hakikisha una kadi ya gari Mara unavyoweka gari lako mtandaoni wateja wengi wataanza kukutafuta. Kabla haujaanza kutangaza mtandaoni hakikisha gari yako unavielelezo vyote kuwa wewe ndio mmiliki pia lipia mapato yako yote ikiwa kama unadaiwa 2.Elewa kipi unakijua kuhusu gari yako Mara mtu anapoanza kukutafuta huwa anakuja na maswali mengi utafanya  vizuri kuwajibu Ikiwa hauna ujuzi wowote ni muda sasa wakuanza kufuatilia gari yako ina engine ya aina g...