Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Siri za mafanikio

 


Nanachoamini mimi, kufanikiwa kweli ni kutimiza malengo yako kwa ufanisi na kwa wakati, lakini mafanikio hayo yakupe amani moyoni mwako (peace of mind).


Vinginevyo, utafanikiwa kwa mrundikano wa fedha huku ukitengeneza tatizo kubwa zaidi la msongo wa mawazo na ukosefu wa amani ya moyo. Hivyo, mafanikio ya njia ya mkato ni mafanikio feki yanayokuja na matatizo mengi mazito zaidi.


Kwa utangulizi huo mrefu, naamini utanielewa zaidi napokupitisha kwenye hizi ‘siri za wazi’ za mafanikio ya kweli katika maisha.


1. Jiamini


Mafanikio ya kweli yanaanza na wewe. Hivyo, kujiamini ni msingi mzuri utakaokufanya utambue uwezo wako katika kufanya jambo fulani. Amini uwezo wa kufanya jambo hilo uko mikononi mwako. Usijishushe, jipime kwa mengi mazuri unayoweza kufanya, ikatae roho ya kujiona huwezi.


2. Thubutu


Neno hili pia ni msingi wa pili mkuu wa mafanikio. Uoga wa kuthubutu ni kikwazo kikuu kinachowarudisha wengi nyuma na kujikuta hata kuanza safari ya mafanikio hawawezi. Jambo lolote zuri na kubwa huwa gumu kufanya na ni rahisi kuhisi haliwezekani. Usikubali kushindwa bila kujaribu. Thubutu kwa dhati na weka nguvu yako na akili yako yote katika uthubutu huo. Hata hivyo, katika uthubutu huu, unapaswa kupima vizuri ili uchukue ‘calculated risk’ na sio ‘just risk’.


3.3. Panga na tekeleza kwa vitendo


Kumbuka, ukishindwa kupanga ujue umepanga kushindwa. Kuwa na mipango inayopimika na kutekelezeka kwa kiwango cha juu. Usiwe na mipango tu mikubwa ambayo hata utekelezaji wake hauwezekani. Unapopanga fikiria wapi utapata rasilimali na jinsi ya kutelezeka, lakini pia mpango wako ukupe uwezo wa kuutathmini na kujipima mwisho wa kazi hiyo. Hata hivyo, mipango haitakuwa na maana kama hautaitekeleza kwa ufanisi. Ukishindwa kutekeleza mpango wako, rudi angalia ulipoteleza ili urekebishe na sio kuufuta mpango mzima bila sababu za msingi.


4.Tengeneza mtandao na wasiliana


Mtandao ni kama daraja au miundombinu ya kuyafikia mafanikio. Hakikisha haujifungii kwenye dunia yako peke yako. Hakikisha kila unaekutana naye na kupata nafasi ya kumfahamu kama mtu anayeweza kuwa sehemu ya daraja bora kwa namna moja au nyingine, anakuwa sehemu ya mtandao wako.


Lakini kuwa na mtandao wa watu pekee hautoshi kama hautawasiliana nao. Kuwasiliana na mtandao huo ni kuufanya uwe ‘active’ ili isionekane kama unawatafuta wakati ukiwa na shida tu. Aidha, unapaswa kujipima kwa kuangalia watu wangapi wanakufahamu wewe zaidi ya watu wangapi unaowafahamu. Kwa mfano: wewe unamfahamu Mkurugenzi wa kampuni ‘A’, Jiulize, je, yeye anakufahamu? Kama hakufahamu basi yeye sio sehemu ya mtandao wako.


Lakini pia, angalia mawasiliano yako ya siku, wangapi umeongea nao kuhusu wazo la biashara au kazi.


5.Kuwa mweli na Mwaminifu


Hii ni siri kubwa zaidi ya zote, japokuwa nimeiweka mwishoni kati ya hizi tano. Usipokuwa mwaminifu na mkweli huku unaona mambo yako yanaenda vizuri unapaswa kushtuka mapema. Wewe ni kama mtu anaevuka ng’ambo ya pili huku akilivunja daraja. Mwisho wa siku utajikuta unaporomoka kabla hujafika unakotakiwa kufika.


Uaminifu utaimarisha mtandao wako kwa hali ya juu zaidi na utatafutwa kwa kuwa wewe utakuwa sehemu ya sababu ya mafanikio ya watu wengine. Kwa mfano, angalia namba ulizonazo kwenye simu yako ya mkononi. Je, ukitaka kumpigia simu dereva taxi majira usiku au hata muda wa kawaida utatumia vigezo gani? Bila shaka uaminifu na ukweli vitatangulia zaidi.


Kuwa mwaminifu na mkweli kwa kila mtu utakayefanya nae kazi, biashara au hata wakati mnafanya mambo ya kawaida ya kijamii kunakupa nafasi ya kuwa chaguo la kwanza kwa watu wanapohitaji huduma, bidhaa au rasilimali ambayo unayo.


Ukifuata kwa uhakika haya matano huku ukimkumbuka Mungu wako kwa kila jambo utafanikiwa kweli na kubaki na amani ya moyo.


Amini katika kile unachoamini na kifanyie utafiti kujiridhisha kabla haujakubali kuyumbishwa kwa tamaa za haraka haraka ili uwe na sababu za kutosha za kukataa au kukubali jambo lolote.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Njia mbalimbali za kuandika tangazo la biashara

Ikiwa ni mfanyabiashara jifunze jinsi ya kuwashawishi wateja na kupata matokeo.unatakiwa kutangaza kupata matokeo makubwa watu wavutiwe na bidhaa zako na kuwafanya wateja kuwa na hamu kubwa ya kununua bidhaa zako Jifunze njia mbalimbali za kuandika tangazo la kuuza bidhaa/huduma mtandaoni 1.Andika kama vile jinsi unavyoongea Kampuni yako au bidhaa yako ni kama mtu na inasifa yakuwa na sauti. Na tumia hiyo sauti kuifuatisha Andika tangazo kama vile unavyoweza kuzungumza,maneno utayoandika kati ya kampuni yako na mnunuzi wako Sauti yako na hasa maneno utayochagua kutumia yatakuwa tofauti sana 2.Andika sifa na faida kabla haujaanza Watu hawawezi kununua bidhaa yako au huduma yako ikiwa hawafahamu watanufaika na nini kwenye bidhaa yako. Mfano unauza  printer waelimishe watu huduma yako itawasaidiaje, je inaokoa mda na kazi? Ubora wa hiyo bidhaa yako? Unamwambia nini mteja ategemee kwenye hiyo bidhaa? Andika sifa na faida kwa mteja kile ambacho atanufaika kuhusu bidhaa au hu...

Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi ya mafuta kwa wateja wa jumla

Makampuni mengi lengo lao kubwa ni kuuza bidhaa zao za mafuta ya ngozi jumla kwa wateja wanaoenda kuuza rejareja. Hatua hii inaweza kuwa changamoto kwa wazalishaji wa bidhaa na wauzaji ili uweze kufanya mauzo vizuri na ufanikiwe kuwapata wanunuzi wa bidhaa yako inatakiwa ufanye maandalizi na ujue nini unategemea Kufanikiwa kufikisha na kuuza bidhaa za mafuta ya ngozi kwa wanunuaji fuata hatua chache na kuwa na ujuzi .kiujumla kampuni inaweza kuwa kubwa ,ikawepo mtandaoni lakini watu wangapi nao wanafanya hivyo Weka mipango vizuri kuhusu wateja,ushindani,na brand izidi kukuwa. Pia kuwa makini wakati wa kuuza na kufanya mapatano ya bei. Mwisho biashara yako itakuwa na itapanuka Mambo yakuzingatia unapotaka kuuza mafuta ya ngozi kwa bei ya jumla 1. Wanunuaji huwa wanaangalia bidhaa yenye ubunifu Inatakiwa uuze bidhaa ambayo mtu atataka kununua . Pengine inaweza ikawa na ubunifu katika kifungashio,vitu vilivyotumika kutengenezea,technolojia,inavyotumika etc  inatakiwa uongeze t...

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni

Kuna watu wengi wanauza magari kupitia mtandao wanatangaza biashara kupitia mitandao mikubwa hapa Tanzania kama guliostore.com , Kupatana na ZoomTanzania, na   ni njia ya kupata wateja wengi zaidi baada ya kuchagua tovuti ya kutaka kutangaza biashara  osha gari lako kisha chukua picha nyingi zakupost mtandaoni Kama mteja atakutafuta utamwambia maongezi ya bei utofauti wa bei na wauzaji wenzio itategemea na gari yako ina hali gani Hapa leo tumekuletea mambo yakuzingatia unapotaka kuuza gari used mtandaoni 1.Hakikisha una kadi ya gari Mara unavyoweka gari lako mtandaoni wateja wengi wataanza kukutafuta. Kabla haujaanza kutangaza mtandaoni hakikisha gari yako unavielelezo vyote kuwa wewe ndio mmiliki pia lipia mapato yako yote ikiwa kama unadaiwa 2.Elewa kipi unakijua kuhusu gari yako Mara mtu anapoanza kukutafuta huwa anakuja na maswali mengi utafanya  vizuri kuwajibu Ikiwa hauna ujuzi wowote ni muda sasa wakuanza kufuatilia gari yako ina engine ya aina g...