Ukifanya biashara hizi utapata faida zaidi ya 50000 kwa siku
1.Biashara ya kuuza samaki
Biashara hii inafaa zaidi kuifanya kwenye majiji makubwa
Tafuta meza maeneo yenye junction au karibu na kituo cha daladala, (eneo lililochangamka kama Mbagala, Buguruni etc)
Nenda ferry kanunue Pweza, ngisi na kamba. Wapike kwa ustadi wa hali ya juu, tumia akili zote kuja na kitu kinachovutia. Uza Supu ya pweza etc, nakuhakilishia, utapata faida zaidi ya 25% ya mtaji wako!
Ukishapata uzoefu, fanya branding kabisa, tafuta kibanda kidogo, kitengeneze vizuri, weka bango andika supu ya pweza! Utapata wateja wa kutosha sana!
2.Biashara ya kuuza mkaa
biashara ya mkaa mkuu hautojutia, kama upo karbu na handeni unaweza fanya proces za kuchoma mkaa angalau uanze na gunia 150 ambapo gharama za kuchoma sio chini ya laki5 na gharama za kusafirisha mpaka dar kila gunia ni 6k
kibali cha tfs laki mbil kwa mwaka
gharama za kibanda hapa dsm unaeza pata kuanzia elf 30 mpk 40 kwa mwez kodi ya pango
kila gunia hapa dsm lnauzwa elfu 25 mpka 30 kama ukibahatika kuuza gunia 3 au 4 kwa siku hyo utakuwa na faida ya uhakika
25000*4=100k
faida katika kila gunia ni sh 10k mpk 15k
3. Biashara ya kuuza mazao ya chakula
Biashara ya nafaka inalipa. unaweza jikita na mazao kama maharagwe, kunde, njegere, mbaazi nk. mtaji unategemea na uhitaji, anza hata kidogo kwa gunia kama 3 kwa kila zao ila fanya utafiti wa soko ili utakapotaka kujitanua isikupe tabu.
Pia unaweza kuyaongezea thamani hayo mazao kama vile kugred na kupark kabisa. Hapo utakuwa umeongeza thamani na utauza kwa bei ya juu, na unaweza tafuta hata supermaket tano tu za kuwa sambazia
4. Biashara ya kuuza viatu vya mtumba
Hii ni biashara pia yenye faida kubwa inayoweza kukutajirisha na kukutoa kabisa kwenye hali ngumu. Biashara hii inahitaji mtaji mdogo tu kuanzia Tsh 50000-1000000
Masoko ya viatu vya mtumba unakoweza kupata kwa bei nzuri ni dar maeneo ya karume kiatu utakachonunua kwa Tsh 5000 utauza mpaka Tsh 20000-30000 hapa utaona ni namna gani biashara hii inafaida
5.Biashara ya kuuza juisi ya miwa
Kuanza biashara hii mambo yafuatayo ni ya msingi kuzingatia:
1) Mashine ya kukamua miwa – Tsh 300,000-400,000
2) Glasi nzuri za ujazo tofauti – Tsh 20,000
3) Chujio – Tsh 5,000
4) Beseni – Tsh 8,000
6) Ndoo 2 – Tsh 5,000
7) Jaba kubwa la uchafu – Tsh 12,000
8) Mtaji wa kununua miwa –Tsh 50,000
9) Tolori la kusafirisha – Tsh 60,000
10) Vifaa vingine – Tsh 40,000
Jumla ya mtaji wa kuanzia Tsh 640,000/=
Muwa mmoja unaweza ukatengeneza lita 4 za juisi na muwa mmoja unaweza ukaununua kwa Tsh.300/= kwa bei ya jumla. Lita moja ya juisi utauza 1,000/= hivyo kwa muwa mmoja unatengeneza Ths 4,000/=.
6. Biashara ya kuuza chips
Maoni
Chapisha Maoni