Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

biashara ya nguo za mitumba

 Balo la nguo mengi huanza kuanzia 380,000 mpaka 480,000 au 520,000 inategemea na ulipo, mzigo unabeba pisi 100 hadi 250 kwa balo. Mtaji uwe tu na hiyo 500,000 kwa balo. Uzia hata chumbani. Mambo yataenda. Mabelo ya kiume mara nyingi mabelo huwa yana anzia 350 na kuendelea, ila kwa kukushauri huko ulipo kama unataka kununua nenda na mtu ambaye anajua hiyo biashara ili akuchagulie belo zuri, coz kuna lebal za kuchukua sio kila mzigo unachuka, zingatia hilo coz wanaweza kusema wamekupa namba moja kumbe sio. Mfano wa lebel nzuri ni hiyo kwenye picha chini hapo. Ushauri! kwanzaa angalia kama eneo lako kuna hali gan ya hewaa kama ni baridi kachukue "shifoni" ni 180000 Mahali wanako uza ni pale mnazi mmojaa mtaa wa sofiaa!! nenda kafanye survey pia ukiwa unatolea mzigo!!! 

Orodha ya biashara za kufanya kwa mtaji mdogo na mkubwa

  Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha. Kutengeneza na kuuza tofali Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.  Kuanzisha kituo cha redio na televisheni Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k Kushona na kuuza nguo. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali, Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza. Kusajili namba za simu na kuuza vocha Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta Kilimo cha maza...

Mambo yakuzingatia unapotaka kuanzisha biashara ya chakula (mgahawa)

  Mgahawa ni moja kati ya biashara zinazolipa hapa nchini. Kutokana na hilo, hakuna urahisi katika biashara hii kuanzia kwa mmiliki hadi wafanyakazi. Na ili watu wapende kula katika mgahawa wako unatakiwa kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa ikiwa ni pamoja na usafi, muonekano wa mgahawa wako n.k. Kama umeamua kufanya biashara hii zingatia haya: Si kila mtu lazima awe mmiliki wa mgahawa Unapenda kupika? Vizuri, unapenda kula? Vizuri zaidi, unapenda kuburudisha? Jambo zuri lakini hayo yote hayawezi kukufanya uwe na vigezo vya kumiliki  mgahawa. Mambo unayotakiwa kuzingatia ni pamoja na je unapenda kufanya kazi masaa mengi? Unaweza kumudu kutolipwa kwa muda? Unaweza kununua bima ya afya? Na sio kufikiria tu kufungua biashara. Wazo la kuwa bosi ni zuri lakini linakuja na majukumu mengi kuliko unavyoweza kufikiria. ADVERTISEMENT Eneo Kati ya vitu muhimu kwenye biashara hii ni eneo. Hutakiwi kupuuzia swala hili kwasababu eneo likiwa zuri uhakika wa kupata wateja wengi ni mkubwa na k...

Mambo ya kuzingatia unapotaka kuanzisha biashara

  Tunakutana tena leo katika safu yetu ya kuhabarishana habari njema, na mafundisho yatakayokutoa sehemu moja kwenda sehem nyingine kifikra na kiuchumi, napenda kusema tu kusoma tu peke yake haitoshi ila kusoma na kuweka kwenye matendo ulichokisoma ndio msaada mkubwa wa mafanikio yako. Leo tutajadili pamoja mambo manne ambayo unatakiwa kuzingatia kabla hujaanza biashara, huenda ulikuwa una wazo la kuanzisha biashara lakini bado hujui yapi ya kufanya mwanzo kabla ya kuanza biashara. Twende wote hadi mwisho wa makala haya utajifunza kitu; 1. WATU: Kitu cha kwanza cha kuzingatia unapowaza kuanzisha biashara ni watu, nadhani unajua kabisa kuwa huwezi kuanzisha biashara bila kuwepo watu, kumbe watu ndio rasilimali pekee unayoweza kuifikiria kabla hujaanza biashara yako, kwa sababu bila watu hakuna mauzo. Tunapozungumzia watu kwenye biashara tunazungumzia watu wa aina mbili; (A) Wateja wako. (B) Watu wanaofanyabiashara kama yako. WATEJA WAKO - Kitu cha kwanza unapotaka kuanzisha biashara...

Siri za mafanikio

  Nanachoamini mimi, kufanikiwa kweli ni kutimiza malengo yako kwa ufanisi na kwa wakati, lakini mafanikio hayo yakupe amani moyoni mwako (peace of mind). Vinginevyo, utafanikiwa kwa mrundikano wa fedha huku ukitengeneza tatizo kubwa zaidi la msongo wa mawazo na ukosefu wa amani ya moyo. Hivyo, mafanikio ya njia ya mkato ni mafanikio feki yanayokuja na matatizo mengi mazito zaidi. Kwa utangulizi huo mrefu, naamini utanielewa zaidi napokupitisha kwenye hizi ‘siri za wazi’ za mafanikio ya kweli katika maisha. 1. Jiamini Mafanikio ya kweli yanaanza na wewe. Hivyo, kujiamini ni msingi mzuri utakaokufanya utambue uwezo wako katika kufanya jambo fulani. Amini uwezo wa kufanya jambo hilo uko mikononi mwako. Usijishushe, jipime kwa mengi mazuri unayoweza kufanya, ikatae roho ya kujiona huwezi. 2. Thubutu Neno hili pia ni msingi wa pili mkuu wa mafanikio. Uoga wa kuthubutu ni kikwazo kikuu kinachowarudisha wengi nyuma na kujikuta hata kuanza safari ya mafanikio hawawezi. Jambo lolote zuri n...

Vitu vya kufanya ili uwe tajiri

  Ili uwe tajiri... 1. Jifunze kuwaamini watu.  Hutaweza kufikia utajiri kupitia ujasiriamali iwapo kila kitu utafanya mwenyewe. Vitu vingi unavyofanya unahitaji kuwapa wengine wakusaidie na wewe uweke nguvu zako kwenye yale ambayo ni muhimu zaidi. Sasa kama huwezi kuwaamini watu na kuona wanaweza kufanya kazi nzuri, hutaweza kuwapa majukumu yako na badala yake utang’ang’ania kufanya kila kitu peke yako na kuishia kushindwa.  Jifunze kuwaamini watu na wape majukumu ambayo wanaweza kukusaidia. Kufikia utajiri unahitaji msaada wa wengi, jua namna ya kufanya kazi vizuri na watu wengi. 2. Fanya vizuri sana kile ulichochagua kufanya.  Hakuna tajiri ambaye anafanya mambo kwa kubahatisha. Wote ambao wanafanikiwa sana kwenye ujasiriamali wanafanya vizuri sana kile ambacho wamechagua kufanya. Wanaweka juhudi kubwa kuongeza thamani na kutengeneza matokeo bora kabisa. Kwa njia hii watu wanawaamini na kuwategemea kupitia kile wanachofanya.  Jitengenezee jina kwa kufanya viz...

Jinsi ya kufanikiwa katika biashara

  Kuanzisha biashara Tanzania huambatana na changamoto kadhaa kama ukosefu wa mtaji na mkakati dhaifu wa uuzaji. Lakini badala ya kuangalia sababu zinazofanya biashara kushindwa, napenda tujikite katika makala hii kwenye mambo yanayoweza kufanikisha biashara inayoanzishwa. Mawazo haya nimeyagawanya katika dondoo zifuatazo. Tazama biashara za maeneo jirani unayoishi au biashara za watu unaowafahamu. Je, ni mambo gani yaliyofanya biashara hizo kufanikiwa, kubaki vilevile kwa muda mrefu, au hata kushindwa? Ni sababu zipi zimeleteleza matokeo hayo? Kwa hakika kuna sababu nyingi,  zikiwemo sababu binafsi ambazo ziko nje ya uewelewa wetu. Kwa msingi huo hatuwezi tukadai kujua sababu za kila biashara kushindwa. Hata hivyo, napenda tutazame baadhi ya mambo muhimu yanayopelekea biashara kufanikiwa au hata kushindwa. Mkakati dhabiti wa uuzaji. Watanzania wanafahamu kutumia fursa katika kufanya biashara zao. Hii huusisha kufungua biashara katika maeneo yalio na watu wengi, au karibu ya k...